Pata taarifa kuu
MOROCCO-UN-USALAMA-SIASA

Guterres aomba kikosi cha Minurso kuongezewa muda wa mwaka mmoja

Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa, Antonio Guterres, katika ripoti ya Jumatano wiki hii kwa Baraza la Usalama la Umoja wa Mataiafa, ameomba "kuongeza muda wa mwaka mmoja" kwa kikosi kinachosimamia amani katika Sahara ya Magharibi (MINURSO) ili kusaidia kuanza kwa mazungumzo ya kisiasa mnamo mwezi Desemba huko Geneva.

Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa, Antonio Guterres.
Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa, Antonio Guterres. Yuri KADOBNOV / AFP
Matangazo ya kibiashara

"Napendekeza kwa Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa kuongeza mwaka mmoja Ujumbe wa Umoja wa Mataifa MINURSO katika Sahara ya Magharibi hadi Oktoba 31, 2019, ili kumpa nafasi mjumbe wangu kuandaa mazingira mazuri yatakayowezesha mchakato wa kisiasa kusonga mbele ", Bw Guterres amesema katika taarifa yake kwa vyombo vya habari.

"Naomba pande husika na majirani kuja kwenye meza ya mazungumzo kwa nia njema bila masharti," tarehe 5 na 6 Desemba nchini Uswisi kama ilivyoandikwa kwenye mwaliko uliotolewa na mjumbe Horst Kohler mwishoni mwa mwezi Septemba, Katibu Mkuu wa Umoja aw Mataifa amesema pia .

Morocco na waai wa Polisario Front walikubali (tarehe 2 na 3 Oktoba) kushiriki katika "mazungumzo ya awali," amesema Guterres, akibaini kwamba ana imani na jibu kutoka Algeria na Mauritania, nchi mbili ambazo zilialikwa kwenye "meza ya ya mazungumzo" yaliyopangwa kufanyika Geneva.

Duru ya mwisho ya mazungumzo kati ya Morocco na waasi wa Polisario Front ilikuwa mwaka 2012.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.