Pata taarifa kuu
COTE D'IVOIRE-ICC-HAKI

Laurent Gbagbo kuomba kuachiliwa huru

Mahakama ya kimataifa ya Uhalifu (ICC) inatarajia Jumatatu hii Oktoba 1 kufungua vikao muhimu katika kesi inayowakabili aliyekuwa rais wa Cote d'Ivoire Laurent Gbagbo na aliyekuwa waziri wake wa vijana Charles Blé Goudé.

Rais wa zamani wa Cote d'Ivoire Laurent Gbagbo, Januari 28, 2016, wakati wa kesi yake katika Mahakama ya Kimataifa ya Uhalifu Hague (Uholanzi).
Rais wa zamani wa Cote d'Ivoire Laurent Gbagbo, Januari 28, 2016, wakati wa kesi yake katika Mahakama ya Kimataifa ya Uhalifu Hague (Uholanzi). ICC-CPI
Matangazo ya kibiashara

Wawili hawa wanaotuhumiwa uhalifu dhidi ya binadamu wakati wa machafuko yaliyotokea baada ya uchaguzi wa urais wa mwaka 2010, wanaomba kuachiliwa huru. Majaji wataamua miezi ijayo ikiwa kesi dhidi ya wawili hao iendelea au la.

Ni miaka saba sasa Laurent Gbagbo akiwa kizuizini huko Hague.

Ombi hili na Ggagbo mwenye umri wa miaka 73, linakuja akiwa ameweka historia kwa kuwa kiongozi wa juu kuwahi kuzuiwa katika Mahakama hiyo yenye makao yake mjini Hague nchini Uholanzi.

Rais huyo wa zamani, anakabiliwa na mashtaka manne, yote ya ukiukwaji wa haki dhidi ya binadamu, kutokana na vurugu za kisiasa zilizotokea baada ya Uchaguzi tata wa urais mwaka 2010 na kusababisha vifo vya zaidi ya watu 3000.

Mawakili wake wanasema wana uhakika kuwa mteja wao ataachiliwa huru, baada ya upande wa mashitaka kushindwa kubaini iwapo Ggagbo alihusika na makosa hayo.

Raia wa Cote d' Ivoire wanatarajiwa kutazama moja kwa moja, wakati kesi hii itaporejelewa.

Hata hivyo wafuasi wa Laurent Gbagbo na Charles Blé Goudé wameahidi kuja kwa wingi kuwaunga mkono viongozi wao mjini Hague. Baada ya miaka miwili kesi hii ikisikilizwa mashahidi wa mwendesha mashitaka, wanasheria wa watuhumiwa hao wawili wamelazimika kuitisha mashahidi wao kuja kutoa ushuhuda. Lakini wakati wa majira ya baridi mwaka uliopita, watuhumiwa hao walipinga kwa undani hoja na ushahidi wa mwendesha mashitaka, na waliomba majaji kutoa uamuzi wa kuwaachilia huru.

Charles Blé Goudé, mbele ya Mahakama ya kimataifa ya Jinai ICC, Oktoba 2 mwaka 2014.
Charles Blé Goudé, mbele ya Mahakama ya kimataifa ya Jinai ICC, Oktoba 2 mwaka 2014. ICC-CPI
Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.