rfi

Hewani
  • RFI Kiswahili
  • Sikiliza taarifa ya Habari
  • RFI kwa Kifaransa

Angola José Eduardo dos Santos Joao Lourenço

Imechapishwa • Imehaririwa

Mtoto wa rais wa zamani wa Angola aanza mgomo wa kula

media
José Filomeno dos Santos, mtoto wa rais wa zamani wa Angola José Eduardo dos Santos DR

Mtoto wa rais wa zamani wa Angola, José Eduardo dos Santos, ambaye anazuiliwa jela tangu Jumatatu wiki hii mjini Luanda katika kesi ya ubadhirifu, ameanza mgomo wa kula, vyanzo kutoka jela vimesema.


"Anakataa kula tangu Jumanne, familia yake inaleta chakula lakini hali," moja ya vyanzo hivyo kimeliambia shirika la habari la AFP.

Mkurugenzi wa zamani wa Mfuko wa kitaifa wa Angola, Jose-Filomeno dos Santos mwenye umri wa miaka 40 anazuiliwa katika jela la Sao Paulo kwa agizo la ofisi kuu mashitaka.

Jose-Filomeno dos Santos anayefahamika kwa jina la Zenu, alishtakiwa mnamo mwezi Machi mwaka huu kwa madai ya "ufisadi, kujitajirisha kinyume cha sheria, kushirikiana na wahalifu" na kuweza kupitisha mlango wa nyuma akiwa pamoja na washirika wake hadi dola biloni 1.5.

Ni wa kwanza kutoka familia ya rais wa zamani dos Santos kufungwa tangu mrithi wake Joao Lourenço kuchukuwa hatamu ya uongozi wa nchi mwaka mmoja uliopita.