Wachimba migodi 16 watekwa nyara kaskazini mwa Nigeria
Wachimba migodi kumi na sita wametekwa nyara na kundi la wahalifu kaskazini mwa Nigeria, katika eneo linalojulikana kwa visa hivyo ambapo watekaji nyara wamekuwa wakiomba fidia kwa familia za mateka , polisi na wakuu wa eneo hilo wamesema.
Imechapishwa:
Watu hao walitekwa Jumanne usiku walipo kuwa njiani wakirudi kutoka mgodini katika eneo la Birnin Gwari katika Jimbo la Kaduna, msemaji wa polisi Yakubu Sabo amesema.
"Wachimba migodi 16 walikuwa wakisafiri kwa lori wakati walipovamiwa karibu na kijiji cha Bogoma na kundi la wahalifu ambao waliwapeleka mahali pasipojulikana," amesema.
"Wanaume wetu kutoka kitengo cha kupambana na utekaji nyara wamekuwa wakitumika eneo hilo ili kupata na kuokoa mateka."
Kwa mujibu wa Abdullahi Bature, msemaji wa kiongozi wa jadi wa Birnin Gwari, Zubairu Mai-Gwari, kisa hicho cha utekaji nyara kilitokea wakati gari waliokuwemo ilikuwa imeegesh akando ya barabara baada ya kupatwa na tatizo.
"Walitekwa nyara usiku lakini watu watatu miongoni mwa wachimba migodi hao walifaulu kutimka wakati walikuwa wakipelekwa katika kichaka. Watekaji nyara hao wanataka fidia," Bature amesema, akiongeza kuwa watekaji nyara hao waliwasiliana na familia za mateka wakiomba pesa.