Pata taarifa kuu
AFRIKA-AMERIKA-ASIA-ULAYA-FAO-NJAA

FAO: Mabadiliko ya hali ya hewa yaongeza njaa duniani

Ripoti ya pamoja iliyochapishwa na Shirika la Umoja wa Mataifa la Chakula na Kiliomo (FAO) na mashirika mengine manne ya umoja huo yanayohusika na suala hilo inaonyesha kwamba njaa ulimwenguni iliongezeka mnamo mwaka 2017, kwa mwaka wa tatu mfululizo.

La Mauritanie vit actuellement un nouvel épisode de sécheresse qui déstabilise le monde agropastoral selon Mohamed ould Maouloud de l'Union des Forces de Progrès, l'UFP (image d'illustration).
La Mauritanie vit actuellement un nouvel épisode de sécheresse qui déstabilise le monde agropastoral selon Mohamed ould Maouloud de l'Union des Forces de Progrès, l'UFP (image d'illustration). Xavier TESTELIN/Gamma-Rapho via Getty
Matangazo ya kibiashara

Miaka kumi na nane iliyopita, Umoja wa Mataifa ulijitoa hadi mwaka wa 2030 ili kuondokana na njaa duniani.

Lengo hili nzuri linaonekana limekosa mwelekeo. José Graziano da Silva, Mkurugenzi Mkuu wa FAO ameelezea masikitiko yake, akisema "kwa bahati mbaya habari kubwa siyo habari njema ... Kwa mwaka wa tatu, napaswa nitangazie kwamba idadi ya watu wanaokabiliwa na njaa duniani imeongezeka. "

Karibu watu milioni 821 walikabiliwa na njaa ulimwenguni mnamo mwaka 2017, ikilinganishwa na 804 mnamo mwaka 2016. Afrika bado inaendelea kuathirika zaidi ikiwa na asilimia 21 ya watu wanaokula vibaya, Asia inachukuwa nafasi ya pili kwa 11.5 %.

Idadi watu wanaokabiliwa na njaa imerejea kwenye kiwango chake cha miaka kumi iliyopita. Mwelekeo wa kushuka umebadilishwa na FAO inasema hali hiyo imesababishwa na mabadiliko ya hali ya hewa:

"Mwaka huu suala la mabadiliko ya hali ya hewa litazingatiwa zaidi. Ripoti hiyo inaonyesha wazi kwamba mabadiliko ya hali ya hewa, na kutokea kwa majanga mbalimbali ya asili, vimeweka hatarini maendeleo na taratibu za kuondokana na njaa na utapiamlo, "ameongeza José Graziano da Silva.

"Jitihada zetu zinapaswa kuzingatia maeneo ya vijijini ..., " Gilbert Houngbo, Rais wa Shirika la Kimataifa la Maendeleo ya Kilimo, moja ya mashirika ya Umoja wa Mataifa alioandika ripoti hiyo, amesema.

Watoto milioni 151 wakabiliwa na njaa

Kwa sababu ya mabadiliko haya ya hali ya hewa, wakulima wana kazi ngumu. Kwa mfano, katika eneo la Kusini mwa Amerika , ambapo suala la El Niño limeambatana na ukame wa mara kwa mara. Theluthi moja ya nchi ambazo zilipata ongezeko la utapiamlo pia zimeathirika na ukame.

Mashirika hayo yamebaini kwamba watoto milioni 151 wanakabiliwa na njaa.

Hali ilivyo nchini Burundi

Wakati ripoti hiyo ikitolewa na mashirika matano ya kimataifa, hali ya usalama wa chakula imeyagusa pia mataifa ya Afrika hususan Burundi ambayo kuna asilimia 14 ya watu ambao wamejikuta katika hali ya ukosefu wa chakula kama anavyoeleza hapa Apollinaire MASUGURU, Msaidizi wa Mwakilishi wa shirika la FAO nchini Burundi anaehusika na mipango.

“Napashwa kuwaambia kwamba Burundi haipo katika mgogoro wa ukosefu wa chakula ni sehemu ndogo tu ya wananchi ambao wanakabiliwa na uhaba wa chakula na wanakadiriwa kuwa asilimia 15, ni hivyo, Kiwango cha uainishaji wa uhaba wa chakula Burundi ipo katika ngazi ya awamu ya 2, awamu ya 2 ni awamu ya chini ya shinikizo.”

Hivi karibuni Mathieu BAZIRA, naibu katibu wa chama CNDD-FDD mkoani Kayanza akizungumzia njaa nchini Burundi. aliwatolea wito wananchi hususan wafuasi wa chama hicho kukabiliana vilivyo na njaa.

Njaa ikilipuka katika nchi usalama unakuwa umeyumba tena kwa kiwango cha kutisha ; ndio maana tunatoa wito kwa wafuasi wa chama CNDD-FDD kupitia mabaraza ya vijiji ili kila mwanachama popote alipo ajipe lengo la kupiga vita njaa.

Endapo sote tutalitambuwa sawa swala hili na kujishulisha na kupiga vita njaa hakuna shaka kwamba wanachama sote
tutapata maendeleo ».

Wananchi wanaona kuwa mzozo wa kisiasa unaolikumba taifa hilo kipindi hiki unachangia katika halii hiyo kutokana na kwamba baadhi ya wakulima ni miongoni mwa waliokimbia nchi

Hali ya usalama wa chakula imeendelea kuwa tishio kubwa na kutishia mipango ya mashirika ya Umoja wa Mataifa kuhusu kutokemeza ukosefu wa chakula ifikapo mwaka 2030.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.