Pata taarifa kuu
CAMEROON-USALAmA-SIASA

Cameroon: Uchaguzi wa urais utafanyika katika mazingira mazuri

Uchaguzi wa urais wa Oktoba 7 nchini Cameroon utafanyika "katika mazingira mazuri" nchini kote, Waziri wa Mambo ya Ndani wa Cameroon, Paul Atanga Nji, amesema wakati mgogoro ambao umesababisha vifo vingi unaendelea katika maeneo ambako wanakzungumza Kiingereza nchini humo.

Makao makuu ya Bunge la cameroon, Yaounde.
Makao makuu ya Bunge la cameroon, Yaounde. AFP
Matangazo ya kibiashara

Uchaguzi wa urais ya Oktoba 7 utafanyika katika mazingira mazuri na amani nchini kote, "Bw Atanga Nji amesema kwenye radio ya serikali ikikunukuu ripoti" zilizowasilishwa na magavana wa mikoa " .

Kuanzia mwanzoni mwa mwaka 2018, mapigano ya kila kukicha kati ya jeshi na wanaharakati wanaotaka eneo lao kujitenga na kuwa nchi huru yamekuwa yakiendelea katika majimbo mawili kunakozungumza Kiingereza.

Wanaharakati kutoka ameneo hayo tayari wametangaza kwamba uchaguzi wau rais hatufanyika katika maeneo haya.

"Rais ametoa agizo kwa magavana kuchukua hatua (muhimu) ili uchaguzi ufanyike katika wilaya 360 za Cameroon," aamejibu Bw Atanga Nji leo Jumatano.

"Haya ni maagizo ya rais ambayo yatatumika kwa hali na mali," amesema waziri huyo, akiongezea kuwa Rais Paul Biya pia "amewaagiza magavana kuhakikisha kuwa ulinzi wa wagombea wote umezingatiwa."

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.