rfi

Hewani
  • RFI Kiswahili
  • Sikiliza taarifa ya Habari
  • RFI kwa Kifaransa

CAR MINUSCA UN Mauaji

Imechapishwa • Imehaririwa

Kumi na mbili wauawa katika machafuko mapya Bria Jamhuri ya Afrika ya Kati

media
Askari wa Ufaransa wa kikosi cha opereshini Sangaris wakipiga doria katika mji wa Bria, Jamhuri ya Afrika ya Kati mwezi Aprili 2014. © AFP PHOTO / MIGUEL MEDINA

Miili ya watu kumi na mbili, ikiwa ni pamoja na miili ya wanawake kumi, imegunduliwa siku wa Alhamisi kuamkia leo Ijumaa asubuhi huko Bria, Jamhuri ya Afrika ya Kati.


Kwa mujibu wa vyanzo kutoka nchini humo vilivyohojiwa na VOA Afrique, watu hawa waliuawa na kundi la zamani la waasi la Seleka kwa kulipiza kisasi shambulio dhidi ya moja ya misafara yao. Shambulio ambalo linadaiwa kuwa lilitekelezwa na kundi la wanamgambo wa Wakikristo la Anti-balaka kilomita 7 kutoka katika mji wa Bria kwenye barabara inayoelekea Ippy.

Vyanzo hivyo vinasema kwamba watu waliouawa walikua wakimbizi wa ndani kutoka kambi ya PK3, iliyo karibu na kambi ya jeshi la Umoja wa Mataifa nchini humo (Minusca).

Kutokakana na mauaji hayo, watu kadhaa waliokimbia makazi yao wameandamana leo Ijumaa mbele ya kambi ya Minusca wakionyesha uzembe wa kikosi hiki cha Umoja wa Mataifa.

Polisi iliingilia kati na kutawanya waandamanaji hao kwa kutumia gesi za machozi.