Pata taarifa kuu
LIBYA-ITALIA-UFARANSA-USALAMA

Salvini yaigeukia Ufaransa na kuishtumu kwa machafuko Libya

Waziri wa Mambo ya Ndani wa Italia, Matteo Salvini, amesema yuko tayari kurejea "haraka" katika mji wa Tripoli, unaokabiliwa na mapigano. Wakati huo huo Bw Salvini ameishtumu Ufaransa kuchangia katika machafuko yanayoendelea nchini Libya.

Waziri wa Mambo ya Ndani wa Italia, Matteo Salvini, Milan Agosti 28, 2018.
Waziri wa Mambo ya Ndani wa Italia, Matteo Salvini, Milan Agosti 28, 2018. © AFP
Matangazo ya kibiashara

"Italia itaendelea kuwa mshirika mkuu wa mchakato wa amani na usalama katika kanda ya Mediterania," kiongozi huyo wa mrengo wa kulia na mmoja wa vigogo wa serikali ya Italia ameandika kwenye ukurasa wake wa Twitter kuhusu Libya. "Mimi mwenyewe niko tayari kurudi hivi karibuni Libya".

Salvini pia amesema "bila shaka, kuna mtu anayechochea (mapigano ya sasa). Hiyo haitoke kwa bahati mbaya. Kwa hofu yangu mimi, mtu kutokana na sababu za kiuchumi, anakubali kuhatarisha usalama wa Afrika ya Kaskazini na, na kupelekea Ulaya kuwa hatarini".

"Nafikiria mtu ambaye alichochea mapigano wakati hakutakiwa kufanya hivyo, kwa mtu anayeweka tarehe ya uchaguzi bila kukutana na washirika, Umoja wa Mataifa na wananchi wa Libya," ameongeza Bw Salvini.

Jumatatu, Waziri wa Ulinzi wa Italia, Elisabetta Trenta, pia alisema kuhusu "kuhusika kwa Ufaransa katika kuingilia kati ya kijeshi dhidi ya serikali ya Kanali Gaddafi mwaka 2011.

"Ni wazi kwamba nchi hii leo inajikuta katika hali hii kwa sababu kuna mtu mnamo mwaka 2011 aliweka mbele maslahi yake," ameandika waziri, wakati italia imekua ikikosoa Paris katika miaka ya hivi karibuni kwa machafuko nchini Libya na kusababisha wimbi kubwa la wahamiaji wanaoingia Ulaya.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.