Pata taarifa kuu
ZIMBABWE-UCHAGUZI-HAKI

Mahakama ya Katiba kutoa uamuzi wake kuhusu uchaguzi Zimbabwe

Mahakama ya Katiba nchini Zimbabwe inatarajiwa kutoa uamuzi kuhusu kesi iliyowasilishwa na kiongozi mkuu wa chama cha upinzani MDC Nelson Chamisa kupinga matokeo yaliyompa ushindi rais Emmerson Mnangangwa baada ya Uchaguzi Mkuu uliofanyika mwezi Julai.

Rais wa Zimbabwe anayemaliza muda wake Emmerson Mnangagwaaliyetangazwa mshindi katika duru ya pili ya uchaguzi uliofanyika Agosti 12, 2018.
Rais wa Zimbabwe anayemaliza muda wake Emmerson Mnangagwaaliyetangazwa mshindi katika duru ya pili ya uchaguzi uliofanyika Agosti 12, 2018. REUTERS/Philimon Bulawayo
Matangazo ya kibiashara

Jaji Mkuu Luke Malaba amesema uamuzi huo utatolewa saa nane mchana saa za Afrika ya Kati.

Kwa zaidi ya saa 10, Majaji wa Mahakama hiyo waliwasikiliza Mawakili wa upinzani na Tume ya Uchaguzi kabla ya kwenda kuandika uamuzi wao.

Mawakili wa kiongozi mkuu wa upinzani Nelson Chamisa wamekuwa wakieleza namna wizi wa kura ulivyofanyika, na kutaka Mahakama kutupilia mbali ushindi huo.

Mbele ya majaji tisa wa mahakama ya juu zaidi nchini Zimbabwe, wanasheria wa Movement for Democratic Change (MDC) kwa muda mrefu wametaja makosa ambayo, wanaona kuwa yalihusika kuvuruga uchaguzi wa Julai 30, uchaguzi wa kwanza tangu Robert Mugabe kutimuliwa madarakani miezi nane iliyopita.

Nacho chama cha rais Mnangangwa ZANU PF, kinataka kesi hiyo kutupiliwa mbali.

Bw Mnangagwa ambaye alipeperusha bendera ya chama cha Zanu-PF katika uchaguzi wa urais alishinda kwa 50.8% ya kura dhidi ya mpinzani wake Nelson Chamisa, ambaye alipata 44.3% ya kura.

Mahakama inaweza kuthibitisha matokeo, kutoidhinisha na kupiga kura upya au kuagiza kurudiwa kuhesabu upya kwa sauti za kura.

Kukata rufaa kwa chama cha MDC tayari kumesababisha kuahirishwa kwa sherehe ya kutawazwa rais Mnangagwa, ambayo awali iliyopangwa kufanyika Agosti 12. Ikiwa Mahakama itathibitisha ushindi wake, sherehe itafanyika ndani ya saa arobaini na nane baada ya uamuzi wa Mahakama ya Katiba.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.