Pata taarifa kuu
DRC-EU-UN-AFRIKA KUSINI-USHIRIKIANO-SIASA

DRC yatoa onyo kali kwa Umoja wa Mataifa, Umoja wa Ulaya na Afrika Kusini

Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo imeelezea washirika wake kuwa inaweza kujiendeleza bila msaada wao, ushauri wao na maoni yao kwa uchaguzi uliopangwa kufanyika miezi minne ijayo, Desemba 23.

Tume ya Kitaifa ya Uchaguzi (CENI) imeonyesha mashine ya kupigia kura itakayotumika katika uchaguzi wa Desemba 23.
Tume ya Kitaifa ya Uchaguzi (CENI) imeonyesha mashine ya kupigia kura itakayotumika katika uchaguzi wa Desemba 23. © AFP
Matangazo ya kibiashara

Serikali ya Kinshasa inataka kuwaweka "wajumbe maalum" na "waangalizi" wengine mbali na mchakato wa uchaguzi ambao lengo lake kuu ni mabadiliko ya kwanza ya amani nchini DRC.

Kwa sasa, kalenda ya uchaguzi inaonekana kuheshimiwa baada ya rais Joseph Kabila kutangaza kuwa hatowania katika uchaguzi wa urais wa Desemba 23 na kuteuliwa kwa "mshirika" wake wa karibu kupeperusha bendera ya chama tawala cha PPRD katika uchaguzi huo na kabla ya kuchapishwa, Ijumaa, orodha ya muda ya wagombea.

Siku ya Jumatatu wiki hii, serikali ya Kinshasa ilikataa uteuzi wa rais wa zamani wa Afrika Kusini Thabo Mbeki kama "mjumbe maalum" nchini DRC, tangazo ambalo lilipitishwa kwenye vyombo vya habari lakini kamwe halijathibitishwa rasmi na serikali ya Afrika Kusini.

Wakati wa utawala wake (1997-2007), Thabo Mbeki alikubali mikataba ya Sun City kukomesha vita viliyotokea mara mbili nchini DRC (1997-2003).

"Ninaweza kuwambia kuwa hakutakuwa na wajumbe maalum nchini DRC, hata Thabo Mbeki," amesema Barnabé Kikaya Bin Karubi, mshauri wa rais anayehusika na masuala ya kidiplomasia.

Wajumbe hawa "huwa na tabia kujiweka kwenye nafasi ya serikali, hawaheshimu uhuru wa DRC, tunataka kuashiria uhuru wetu," ameongeza Waziri wa Mawasiliano, Lambert Mende.

Mvutano wa kisiasa nchini Drc unaendelea kuhusu matumizi ya machine za kupigia kura, ambapo upinzani umetishia kutoshiriki uchaguzi iwapo machini hizo zitatumiwa katika uchaguzi wa Desemba 23.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.