Pata taarifa kuu
MALI-UFARANSA-SIASA-USALAMA

Macron ampongeza IBK kwa ushindi wake

Rais wa Ufaransa Emmanuel Macron amempigia simu mwenzake wa Mali Ibrahim Boubacar Keïta,("IBK"), akimpongeza kwa ushindi wake katika duru ya pili ya uchaguzi, ikulu ya Elysée imetangaza.

Rais wa Mali Ibrahim Boubacar Keita akimkaribisha Rais wa Ufaransa Emmanuel Macron huko Nouakchott, Mauritania, Julai 2, 2018.
Rais wa Mali Ibrahim Boubacar Keita akimkaribisha Rais wa Ufaransa Emmanuel Macron huko Nouakchott, Mauritania, Julai 2, 2018. © AFP
Matangazo ya kibiashara

Pia "ameelezea ahadi ya Ufaransa kuunga mkono serikali na raia wa Mali ili kukabiliana na changamoto ya vita dhidi ya ugaidi na kukuza uwekezaji na maendeleo ya kiuchumi."

Rais anayemaliza muda wake Ibrahim Boubacar Keïta, mwenye umri wa miaka 73, alichaguliwa katika duru ya pili ya uchaguzi wa urais Agosti 12 kwa muhula wa pili, ushindi ambao wafuasi wake wanaendelea kusherehekea lakini upinzani umetupilia mbali matokeo hayo, hata kabla ya matokeo hayo kutangazwa hapo Alhamisi wiki hii.

IBK alishinda kwa 67.17% ya kura katika duru ya pili ya uchaguzi wa Agosti 12, dhidi ya mpinzani wake Soumaïla Cissé, mwenye umri wa miaka 68, ambaye alipata 32.83% ya kura. Kiwango cha wapiga kura walioshiriki uchaguzi huo kilikua cha chini kabisa: 34.54%.

Rais wa zamani François Hollande pia amempongeza Ibrahim Boubacar Keita kwa kuchaguliwa tena kwa muhula wa pili mfululizo. "Nimempongza na kumuomba kuwaweka pamoja raia wa Mali kama sehemu ya mkataba wa amani na kuhakikisha usalama na maendeleo kwa wote," Bw Hollande alisema katika taarifa yake siku ya Alhamisi.

Paris inafuatilia kwa karibu hali nchini Mali, ambako tangu mwaka 2012 ilituma kikosi kikubwa zaidi cha askari wake wanaohudumu nje ya nchi.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.