Pata taarifa kuu
COMORO-SIASA-USALAMA

Wapinzani waendelea kukamatwa Comoro

Nchini Comoro chini ya wiki mbili baada ya kufanyika kwa kura ya maoni, wapinzani wameendelea kukamatwa na maafisa wa usalama na kuzuiwa. Mashirika ya Haki za Binadamu nchini humo yamemeendelea kukosoa hatua hiyo ya serikali.

Zoezi la kupiga kura huko Moroni, Comoro, wakati wa kura maoni kuhusu marekebisho ya katiba Julai 30, 2018.
Zoezi la kupiga kura huko Moroni, Comoro, wakati wa kura maoni kuhusu marekebisho ya katiba Julai 30, 2018. TONY KARUMBA / AFP
Matangazo ya kibiashara

Mwandishi na mwanaharakati maarufu Said Ahmed Said Tourqui, anayefahamika kwa jina lingine kama Sast, amekamatwa pamoja na ndugu yake mmoja.

Me Bahassane Said Ahmed, kaka wa Makamu wa rais wa zamani pia amekamatwa baada ya kupinga kura hiyo ya amani.

Kura ya ndio ilishinda na hivyo kumpa nafasi rais Azali Assoumani kuwania tena kwa mihula miwili, lakini pia iliondoa wadhifa wa makamu wa rais na kuondoa Mahakama ya kikatiba.

Kura hiyo ya maoni ilisusiwa na upinzani, ambao licha ya kutoshiriki, umedai kuwa kulikuwa na wizi mkubwa wa kura.

Kabla ya kufanyiwa marekebisho, Katiba ya Comoro ilipigiwa kura mwaka 2001, ilimtaka rais kuongoza kwa muhula mmoja wa miaka mitano huku akitokea katika visiwa vitatu vidogo vya Kisiwa hicho.

Hata hivyo, marekebisho ya Katiba hiyo yaliondoa kipengele hicho na sasa, rais anaweza kutoka katika eneo lolote la kisiwa hicho.

 

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.