Pata taarifa kuu
ETHIOPIA-SIASA-USALAMA

Ethiopia na waasi wa OLF watia saini mkataba wa kumaliza uhasama

Serikali ya Ethiopia na kundi moja kuu la waasi nchini humo Oromo Liberation Front- OLF wametia saini muafaka wa amani ili kumaliza uhasama uliokua ukiendelea nchini humo.

Waziri Mkuu wa Ethiopia Abiy Ahmed akijibu maswali ya wabunge huko Addis Ababa,Aprili 19, 2018.
Waziri Mkuu wa Ethiopia Abiy Ahmed akijibu maswali ya wabunge huko Addis Ababa,Aprili 19, 2018. REUTERS/Tiksa Negeri/File Photo
Matangazo ya kibiashara

Hatua hii inatajwa kama jitihada za waziri mkuu mpya wa nchi hiyo Abiy Ahmed kutatua migogoro iliyodumu kwa muda mrefu ndani ya taifa hilo la pili Afrika kwa idadi kubwa ya watu.

Kwa mujibu wa Runinga ya taifa nchini Ethiopia mkataba huo umesainiwa katika mji mkuu wa Eritrea ambapo ndio makao makuu ya kundi la waasi la OLF.

Makubaliano hayo yanaonyesha hatua nyingine anayopiga Waziri mkuu Abiy Ahmed, ya kufanyia mabadiliko taasisi mbali mbali za taifa hilo, kupanua uchumi, pamoja na kuboresha usalama na uhusiano wa kidiplomasia na mataifa mengine duniani.

Waziri wa habari wa Eritrea Yemane Gebremeskel amesema kwa sasa OLF itatumia njia za amani kujishughulisha na masuala ya siasa nchini Ethiopia.

Mapema wiki hii serikali ya Ethiopia ilitangaza kuwa sasa kundi hilo halitaitwa la kigaidi kama ilivyokuwa ikijulikana hapo awali.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.