Pata taarifa kuu
DRC-KATUMBI-SIASA-HAKI

Moise Katumbi aapa kurejea DRC kabla ya Agosti 8

Mwanasiasa wa upinzani na Gavana wa zamani wa jimbo la Katanga nchini DRC Moise Katumbi ambaye amekwama nchini Zambia baada ya kuizuiwa na maafisa wa nchi yake kurudi nyumbani, amesisitiza kuwa ataendeleza najuhudi za kuvuka mpaka na kuingia DRC.

Moise Katumbi bado amekwama nje ya nchi.
Moise Katumbi bado amekwama nje ya nchi. © Federico Scoppa/AFP
Matangazo ya kibiashara

Katumbi amesema ni lazima, arejee nyumbani kabla ya siku ya Jumatano ili kuwasilisha ombi la kuwania urais, kabla ya siku ya mwisho ambayo ni tarehe nane.

Mwishoni mwa wiki iliyopita, mwanasiasa wengine wa upinzani Jean Pierre Bemba ambaye alirejea jijini Brussels alishtumu hatua ya serikali ya Kinshasa kumzuia Katumbi kurudi nyumbani.

Moise Katumbi, ameendelea kupinga amri ya serikali ya rais Joseph Kabila ya kumpiga marufuku kurudi kwake nchini DRC kutoka uhamishoni Afrika Kusini, kwa kuwa ni kinyume na haki za binadamu.

Gavana huyo wa zamani wa Jimbo la Katanga alipanga kurudi nchini mwake akipitia mjini Lubumbashi, ili kuchukua fomu ya kuwania katika uchaguzi wa urais, lakini hajapewa ruhusa ya ndege yake kutua katika ardhi ya DRC.

Aidha, vyombo vya habari nchini DRC vimeripoti kuwa, Moise Katumbi na washirika wake wanaonekana kupuuzia marufuku ya serikali hiyo, lakini ndege yake binafsi haijapewa ruhusa ya kutua.

Katika barua yake, Meya wa Jiji la Lubumbashi, Ghislain Robert Lubaba Buluma, amesema kuwa ndege ya Moise Katumbi imekataliwa kutua au kupaa katika anga ya DRC.

“Moise Katumbi anakabiliwa na mashitaka ya kuajiri askari mamluki kwa lengo la kuangusha utawala wa Rais Joseph Kabila,” vyanzo kadhaa vya serikali vimeeleza.

Hata hivyo, hatua hiyo imewashangaza wanasheria wa mwanasiasa huyo, ambao wamesema kesi hiyo ilikuwa ikisubiriwa kusikilizwa baada ya kukata rufaa.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.