Pata taarifa kuu
DRC-EBOLA-AFYA

Waziri wa Afya wa DRC azuru Kivu Kaskazini

Waziri wa Afya wa DRC amezuru Beni, mashariki mwa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo, Alhamisi wiki hii, eneo lililoathirika na maambuki mpya ya Ebola ambayo yamesababisha vifo vya watu 20, kwa muijbu wa viongozi husika.

Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo (DRC) yaendelea kukumbwa na maambukizi ya virusi vya Ebola.
Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo (DRC) yaendelea kukumbwa na maambukizi ya virusi vya Ebola. REUTERS/Kenny Katombe
Matangazo ya kibiashara

"Ujumbe unaongozwa na Waziri wa Afya uliwasili Beni Alhamisi wiki hii" kuandaa makabiliano dhidi ya virusi vya Ebola katika mji huu ambao tayari uko chini ya tishio la kundi la watu wenye silaha, Naibu Meya, Modeste Bakwanamaha, ameliambia shirika la habari la AFP.

Waziri Oly Ilunga amesema siku moja kabla kuwa DRC inakabiliwa na maambukizi mapya ya ugonjwa huo, wiki moja tu baada ya kutangazwa kutokomezwa kwa maambukizi ya awali ya Ebola kaskazini-magharibi mwa nchi.

Mkoa wa Kaskazini Kivu ulifahamisha Jumamosi "Wizara ya Afya kesi 26 za maambukizi ya ugonjwa wa Ebola, ikiwa ni pamoja na vifo vya watu 20," alisema waziri huyo, bila ya kutoa maelezo zaidi kuhusu tarehe ambapo vifo hivyo vilitokea.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.