rfi

Hewani
  • RFI Kiswahili
  • Sikiliza taarifa ya Habari
  • RFI kwa Kifaransa

Mali Ibrahim Boubacar Keita Antonio Guterres

Imechapishwa • Imehaririwa

Wapigakura milioni nane kushiriki uchaguzi mkuu nchini Mali

media
Uchaguzi mkuu unafanyika leo jumapili nchini Mali REUTERS/Luc Gnago

Zaidi ya raia milioni nane nchini Mali wanapiga kura jumapili katika uchaguzi muhimu kwa taifa hilo la Sahel ambalo limekabiliwa na usalama mdogo kutokana na mashambulizi kutoka kwa makundi ya kijihadi.


Raisi wa Mali Ibrahim Boubacar Keita,mwenye umri wa miaka 71,ni miongoni mwa wagombea 24 akiwemo mwanamke mmoja wanaowania kiti cha uraisi.

Raisi Keita amekuwa akikosolewa na wapinzani wake kwa kushindwa kurejesha usalama lakini na hata waliokuwa mawaziri wake ambao walisema raisi huyo ameshindwa kiusalama.

Kwa upande wake Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Antonio Gutereres amesema anatiwa moyo na jinsi ambavyo kumekuwepo na amani wakati wa kampeni licha ya changamoto za usalama kwenye maeneo ya kaskazini na kati mwa taifa hilo la Mali.

Amewataka wapiga kura katika taifa hilo lenye takribani  watu milioni 18, wajitokeze kwa wingi kumchagua kiongozi wanaompenda katika hatua hiyo muhimu ya kidemokrasia.