Pata taarifa kuu
ETHIOPIA-MAREKANI-USHIRIKIANO

Waziri Mkuu wa Ethiopia azuru Marekani

Waziri Mkuu wa Ethiopia Abiy Ahmed anazuru Marekani Alhamisi wiki hii, ikiwa ni ziara yake ya kwanza tangu alipoingia madarakani mwezi Aprili. Ziara hiyo ya siku sita, itampeleka kiongozi huyo wa Ethiopia jijini Washington DC na Los Angeles.

Waziri Mkuu wa ethiopia Abiy Ahmed, katika ziara yake nchi Marekani atakutana na wananchi wa Ethiopia waishio nchini humo.
Waziri Mkuu wa ethiopia Abiy Ahmed, katika ziara yake nchi Marekani atakutana na wananchi wa Ethiopia waishio nchini humo. REUTERS/Tiksa Negeri/File Photo
Matangazo ya kibiashara

Ziara hiyo ya siku sita, itampeleka kiongozi huyo wa Ethiopia jijini Washington DC na Los Angeles.

Anatarajiwa kukutana na raia wa Ethiopia wanaoishi nchini humo na kuwaeleza juhudi anazofanya kuwaunganisha Waethiopia na kuwashawishi kurudi nyumbani.

Abiy Ahmed amekua akijaribu kufufua uhusiano wa kidiplomasia na nchi jirani ya Eritrea, baada ya hivi karibuni kutoa taarifa ya pamoja ya amani na urafiki na kubaini kwamba muda umewadia sasa wa kuboresh amaridhiano na Eritrea.

Abiy Ahmed amemrithi mtangulizi wake Hailemariam Desalegn, ambaye alijiuzulu mnamo mwaka huu kufuatia mvutano wa kisiasa nchini humo.

Wiki jana rais a Eritrea Isaias Afwerki alifanya ziara ya kihistoria nchini Ethiopia na mataifa hayo mawili yaliandika historia kwa kuanzisha uhusiano mpya.

Rais Afwerki alizuru Addis Ababa katika ziara, wiki moja baada ya mataifa hayo mawili kutangaza kusitisha vita ambavyo vimekuwa vikiendelea kwa zaidi ya miaka 20.

Waziri Mkuu wa Ethiopia Ahmed Abiy, wiki mbili zilizopita alikuwa Asmara na ikakubaliwa kuwa mataifa hayo jirani ambayo zamani yalikuwa nchi moja, kuanza kushirikiana katika nyanja mbalimbali.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.