Pata taarifa kuu
NIGERIA-BOKO HARAM-USALAMA

Wafanyabiashara sita wauawa katika shambulizi la Boko Haram Nigeria

Boko Haram imeua raia sita katika shambulizi la kuvizia dhidi ya msafara wa magari yaliyokua yakibeba bidhaa mbalimbali, magari ambayo yalikua yakisindikizwa na jeshi kaskazini-mashariki mwa Nigeria, kwa mujibu wa vyanzo vya kuaminika.

Uharibifu unaofanywa na Boko Haram, Nigeria.
Uharibifu unaofanywa na Boko Haram, Nigeria. http://allafrica.com
Matangazo ya kibiashara

"Wafanyabiashara sita wameuawa katika shambulizi la kuvizia la Boko Haram," Umar Kachalla, mwanachama wa kundi la kiraia la wanamgambo linaloshirikiana na jeshi la serikali katika vita dhidi ya Boko Haram.

Shambulizi hilo lilitokea Jumanne jioni, kilomita kumi na tano kutoka mji wa Gamboru, kwenye mpaka na Cameroon.

Washambuliaji walifyatulia risasi msafara wa magari 23, wakiyalazimisha kusimama, kabla kuiba bidhaa na kuchoma moto magari, amesema Bw kachalla.

"Kutokana na hali ya barabara, ni vigumu kwa madereva kuepuka mashambulizi ya kuvizia kwenye barabara hiyo kwa sababu wanatakiwa kuendesha magari pole pole kutokana na mashimo kwenye barabara hiyo," Be Kachalla ameongeza.

Mashahidi wanasema magari yote yaliteketea kwa moto, kinachobaki tu kwenye barabara hiyo ni jivu.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.