Pata taarifa kuu
COTE D'IVOIRE-SIASA-USALAMA

Uchaguzi wa serikali za mita kufanyika Oktoba 13 Cote d'Ivoire

Uchaguzi wa serikali za mitaa na ule wa wakuu wa majimbo utafanyika Oktoba 13 Cote d'Ivoire, serikali imesema Alhamisi wiki hii katika taarifa yake.

Afisa wa uchaguzi akiweka muhuri kwenye kadi ya kupigia kura ya mpiga kura ambaye amepiga kura katika uchaguzi wa wabunge huko Abidjan, Côte d'Ivoire, Desemba 18, 2016.
Afisa wa uchaguzi akiweka muhuri kwenye kadi ya kupigia kura ya mpiga kura ambaye amepiga kura katika uchaguzi wa wabunge huko Abidjan, Côte d'Ivoire, Desemba 18, 2016. REUTERS/GHIDEON MUSA ARON VISAFRIC
Matangazo ya kibiashara

"Kwa pendekezo la Tume Huru ya Uchaguzi,"agizo la serikali " linaitisha uchaguzi siku ya Jumamosi, Oktoba 13, 2018, kwa minajili ya kuwachagua madiwani wa mikoa na madiwani wa wilaya," ilisema taarifa hiyo.

Kwa miezi kadhaa, tarehe halisi ya uchaguzi ilikua ikisubiriwa kwa hamu na gamu.

Tangazo hili linakuja huku kukiwa na mvutano wa kisiasa, siku tatu baada ya uzinduzi wa "chama kuunganishwa kwa chama kimoja" na rais waCote d'Ivoire, Alassane Ouattara.

Mungano wa vyama vinavyotembelea sera ya hayati rais Félix Houphouët-Boigny wa RHDP uliokutana mjini Abidjan, mapema wiki hii ulimteua rais Alasasane Ouattara kuwa kiongozi wa mmungano huo. RHDPinajumuisha vyama vya RDR, (chama cha Rais Ouattara), na viongozi wa kisiasa kutoka vyama vingine kadhaa.

Lakini chama cha Democratic Party of Ivory Coast (PDCI), ambacho ni mshirika mkuu wa RDR katika muungano madarakani, kimekataa kujiunga na muungano wa RHDP, kukisema hakikifurahia masharti ya muungano yaliyopendekezwa.

Mbali na uchaguzi wa serikali za mitaa wa mwezi Oktoba, wanasiasa mbalimbali wameapa kuwania katika uchaguzi wa urais uliyopangwa kufanyika ndani ya kipindi cha miaka miwili.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.