Pata taarifa kuu
ETHIOPIA-ERITREA-SIASA

Rais wa Eritrea afanya ziara ya kihistoria nchini Ethiopia

Rais a Eritrea Isaias Afwerki amefanya ziara ya kihistoria nchini Ethiopia na mataifa hayo mawili yanaandika historia kwa kuanzisha uhusiano mpya.

Rais wa Eritrea Isaias Afwerki (kushoto) na Waziri Mkuu wa Ethiopia Abiy Ahmed (kulia).
Rais wa Eritrea Isaias Afwerki (kushoto) na Waziri Mkuu wa Ethiopia Abiy Ahmed (kulia). REUTERS/GHIDEON MUSA ARON VISAFRIC
Matangazo ya kibiashara

Rais Afwerki amezuru Addis Ababa katika ziara inayokuja, wiki moja baada ya mataifa hayo mawili kutangaza kusitisha vita ambavyo vimekuwa vikiendelea kwa zaidi ya miaka 20.

Waziri Mkuu wa Ethiopia Ahmed Abiy, wiki iliyopita alikuwa Asmara na ikakubaliwa kuwa mataifa hayo jirani ambayo zamani yalikuwa nchi moja, kuanza kushirikiana katika nyanja mbalimbali.

Abiy alimkaribisha rais Afwerki katika chakula cha mchana, na walionekana wakicheka pamoja huku kiongozi wa Ethiopia akimwelezea mgeni wake kama mpendwa, mtu anayeheshimiwa na aliyekoswa na wananchi wa Ethiopia.

Naye rais Afwerki amesema kinachoendelea ni historia na raia wa Ethiopia na Eritrea sio wananchi wa mataifa mawili bali ni watu wamoja.

Rais huyo wa Eritrea atakuwa Ethiipia kwa muda wa siku wa siku tatu, ziara ambayo imewakumbusha wengi uhusiano wa karibu wa mataifa hayo mawili, kabla ya Eritrea kujitenga mwaka 1993.

 

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.