Msafara wa Waziri wa Ulinzi wa Cameroon washambuliwa
Msafara wa magari uliokuwa unamsafirisha Waziri wa Ulinzi wa Cameroon Joseph Beti Assomo umeshambuliwa katika eneo ambalo kuna wazungumzaji wa lugha ya Kiingereza.
Imechapishwa:
Ripoti zinasema kuwa, wanajeshi wanne walijeruhiwa huku washambuliaji kadhaa wakiuawa.
Hili ni shambulizi linalokuja, baada ya rais Paul Biya mwenye umri wa miaka 85 kutangaza kuwa atawania tena urais wakati wa Uchaguzi Mkuu mwezi Oktoba.
Kwa muda mrefu sasa, wanaharakati kutoka Kusini mwa nchi hiyo wamekuwa wakishinikiza kujitenga na kuunda taifa lao wanalotaka liitwe Ambazonia.
Hata hivyo, serikali ya Yaounde imeendelea kusisitiza kuwa, Kusini mwa nchi hiyo ni Cameroon na madai ya wanaharakati hayo hayawezi kupewa nafasi.
Maelfu ya raia wa Cameroon wanaozungumza Kiingereza wamekimbilia nchini Nigeria kwa wasiwasi wa kuuwawa kutokana na makabiliano kati ya maafisa wa usalama na wanaharakati.