Pata taarifa kuu
CAMEROON-SIASA-USALAMA

Rais wa Cameroon Paul Biya kuwania muhula wa 7 mwezi Oktoba

Rais wa Cameroon Paul Biya, ambaye yuko madarakani kwa karibu miaka 36 sasa, ametangaza Ijumaa wiki hii kuwa atawania muhula wa saba katika uchaguzi wa urais wa Oktoba 7.

Rais wa Cameroon Paul Biya.
Rais wa Cameroon Paul Biya. REUTERS/Philippe Wojazer
Matangazo ya kibiashara

Rais Biya ana umri wa miaka 85 na muhula wa rais ni wa miaka saba nchini Cameroon.

"Wananchi wenzangu wa Cameroon na wale waishio nchi za kigeni, tunajua changamoto ambazo tunakabiliana nazo kwa Cameroon, yenye umoja, usalama na amani, nakubali kuitikia malalamiko yenu ya haraka, nitakuwa mgombea urais katika uchaguzi ujao wa urais" Paul Biya ameandika kwenye ukurasa wake waTwitter.

Cameroon inaendelea kushuhudia machafuko kutokana na makabiliano ya wanaharakati wanaotaka kujitenga kwa maeneo yao yenye watu wengi wanaozungumza Kiingereza na vikosi vya usalama. Machafuko hayo yameua askari 84 tangu mwezi Septemba mwaka jana kusini magharibi mwa nchi.

Wakazi kutoka maeneo hayo wanapinga kwa mwaka mmoja sasa dhidi ya kile wanachosema kutengwa na kunyanyaswa na serikali ya rais Biya, ambayo ina wajumbe wengi kutoka maeneo kunakozungumzwa Kifaransa.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.