rfi

Hewani
  • RFI Kiswahili
  • Sikiliza taarifa ya Habari
  • RFI kwa Kifaransa

Cameroon Boko Haram

Imechapishwa • Imehaririwa

Uchunguzi waanzishwa kuhusu mauaji ya wanawake na watoto Cameroon

media
(Picha ya kumbukumbu) Askari wa Cameroon walitumia waliotumwa katika ngome ya Mabass. Kijiji kilio karibu na mpaka na Nigeria, karibu na vijiji vinavyodhibitiwa na Boko Haram. RFI/OR

Baada ya video inaonyesha watu wanaoshtumiwa kuwa askari wa Cameroon wakiua wanawake wawili na watoto zao wawili, viongozi wa nchi hiyo wametaka uchunguzi ufanyike ili wahusika wafikishwe mbele ya vyombo vya sheria.


Video hiyo imekua gumzo na kendelea kusambaa kwenye mitandao ya kijamii nchini Cameroon na nje ya nchi hiyo. Uchunguzi umeanzishwa baada ya video hiyo kurushwa kwenye mitandao ya kijamii, video ambayo inaonyesha watu wanaoshtumiwa askari wa cameroon wakiua wanawake wawili na watoto zao wawili wakiwashtumu kuwa wanashirikiana na kundi la Boko Haram.

Katika taarifa kwa vyombo vya habari,siku ya Jumatatu msemaji wa serikali, Issa Tchiroma Bakary, ameshutumu video hiyo kuwa inakuza chuki na kusema kuwa taarifa hiyo ni "habari ya uzushi", huku akibaini kwamba video "imetengenezwa" kwa lengo la kupata matope jeshi la serikali. "Hata hivyo [...] rais wa nchi (Paul Biya) ameagiza uchunguzi ufanyike kwa mujibu sheria," Bw Tchiroma Bakary ameongeza.

Katika video, iliyorushwa Jumanne wiki hii kwenye mitandao ya kijamii, wanaonekana watu waliovaa sare za kijeshi sawa na zile za baadhi ya vitengo vya jeshi la Cameroon wakiwaua wanawake wawili na watoto zao. Kabla ya kuwaua, watu hao, waliwaita kwa Kifaransa "BH" (ikimaanisha Boko Haram) na kuongeza kuwa wanawake hao na watoto zao walikamatwa wakati wa operesheni dhidi ya wapiganaji wa kundi la Boko Haram.

Vyanzo viwili vya usalama nchini Cameroon vimesem akuwa video hiyo ilirekodiwa katika eneo la milima, kaskazini mwa nchini, linalopakana baadhi ya ngome za Boko Haram nchini Naigeria.