rfi

Hewani
  • RFI Kiswahili
  • Sikiliza taarifa ya Habari
  • RFI kwa Kifaransa

Cameroon

Imechapishwa • Imehaririwa

Mapigano makali yazuka Kumba, Kusini Magharibi mwa Cameroon

media
Maofisa wa polisi wa Cameroon katika mtaa wa Buea, kilomita 60 magharibi mwa Douala, Oktoba 1, 2017. © AFP

Watu wengi wameuawa tangu Jumatatu wiki hii katika mji wa Kumba, mji wenye watu wengi wanaozungumza Kiingereza, Kusini Magharibi mwa Cameroon.


Mapigano yalitokea Jumatano usiku na Alhamisi asubuhi wiki hii kati ya jeshi na wanaharakati wanaotaka eneo hilo kujitenga waliokua wakibebelea silaha.

Watu wengi, ikiwa ni pamoja raia wa kawaida, wameuawa katika mapigano hayo huko Kumba tangu siku ya Jumatatu, "chanzo hospitali kimeliambia shirika la habari la AFP, na kuthibitishwa habari iliyotolewa na mashahidi.

Chanzo hicho kimebaini kuwa "watu hao wameuawa katika operesheni mbalimbali za jeshi" kufuatia kuawa siku ya watu kwa kamanda wa polisi katika mji wa Kumba, mauaji yanayodaiwa kutekelezwa na wanaharakati wanaotaka kujitenga kwa maeneo yao.

Tangu kifo cha afisa huyo wa polisi, hali ya usalama imeendelea kudorora katika mji huo.