rfi

Hewani
  • RFI Kiswahili
  • Sikiliza taarifa ya Habari
  • RFI kwa Kifaransa

DRC Joseph Kabila Moïse Katumbi

Imechapishwa • Imehaririwa

Chama cha Moise Katumbi chatishia kutoshiriki uchaguzi

media
Mwanasiasa wa upinzani DRC, Moise Katumbi, ambaye yuko uhamishoni. Getty Images

Chama cha Ensemble pour le changement kinachoongozwa na mwanasiasa tajiri nchini DRC, Moise Katumbi,kimesisitiza kuwa hakitakubali kushiriki katika uchaguzi mkuu wa Desemba 23 2018 ikiwa tume ya uchaguzi CENI itaendelea na mpango wake wa kutumia mashine za kielektroniki.


Wanasiasa wa upinzani wanaojumuika katika chama wameishtumu Tume ya Uchaguzi CENI kwamba imekua ikipata vishawishi kutoka serikali ili iweze kutumia machine hizo za kielektroniki.

Kwa upande wake mwenyekiti wa CENI Corneille Nangaa amesema kuwa Uchaguzi utafanyika kama ilivyopangwa, Desemba 23 mwaka huu, na amerejelea matamshi yake kwamba hakuna uwezekano wa kufanyika kwa uchaguzi nchini humo bila ya kutumia mashine hizo.

Zoezi la kuwaandika wagombea kwenye viti vya ubunge limetamatika wakati kuna taarifa za kuwepo kwa majimbo ambayo ofisi za CENI hazikupokea hata jalada moja kutoka kwa wagombea, mfano wa jimbo la Kasai ya kati.

Mgogoro wa kisiasa unaendelea nchini DRC wakati ikisalia miezi isiyozidi mitano kabla ya uchaguzi mkuu nchini humo, huku raia wakiwa na wasiwasi ya kutokea kwa machafuko kufuatia mgogoro huo.

Vyama kadhaa vya kisiasa vimekua vikitishia kutoshiriki uchaguzi huo iwapo rais anayemaliza muda wake Joseph Kabila atawania muhula mwengine.

Mpaka sasa rais Joseph Kabila hajazungumza chochote kuhusiana na yeye kuwania au la katika uchaguzi huo.