rfi

Hewani
  • RFI Kiswahili
  • Sikiliza taarifa ya Habari
  • RFI kwa Kifaransa
  • Mafuriko yameua watu kumi na nane Iran (idara ya hali ya Dharura)

Afrika Kusini Jacob Zuma

Imechapishwa • Imehaririwa

Mtoto wa Zuma afikishwa mahakamani

media
Duduzane Zuma, mtoto wa aliyekuwa rais wa Afrika Kusini anayeshtumiwa makosa yanayohusiana na mauaji na rushwa. © AFP

Mtoto wa aliyekuwa rais wa Afrika Kusini Jacob Zuma ambaye alirejea nchini Ijumaa ya wiki iliyopita, amefikishwa Jumatatu wiki hii katika mahakama maalum inayoshughulikia kesi za rushwa huko Johannesburg.


Alifikishwa mahakamani, huku miguu yake ikiwa imefungwa mnyororo.

Duduzane Zuma ameachiliwa baada ya kulipa dhamana ya rand 100,000.

Mamlaka imemnyang'anya pasipoti yake.

Mahakama imeahirisha kesi ya mtoto huyo wa Jacob Zuma hadi Januari 24 kwa ajilia ya uchunguzi zaidi.

Tangu baba yake kutimuliwa mamlakani, ni mara ya kwanza vyombo vya shera vya Afrika Kusini kushughulikia kesi yamtoto wa Jacob Zuma anayeshtumiwa kuhusika katika kesi kadhaa.

Duduzane Zuma, ambaye alirejea Afrika Kusini siku ya Ijumaa kuhudhuria mazishi ya mmoja wa ndugu zake, aliwekwa kizuizini kwa masaa kadhaa na polisi katika uwanja wa ndege wa Johannesburg.

Wiki ijayo atafikishwa mahakamani kujibu tuhuma zinazomkabili katika kesi nyingine ya mauaji wakati wa ajali ya gari mwaka 2014 ambapo alimuua mwanamke mmoja na kumjeruhi mtu mwingine ambaye alifariki dunia baadaye. hospitalini.

Hata hivyo Duduzane Zuma amefutilia mbali tuhuma dhidi yake katika ajali hiyo.