rfi

Hewani
  • RFI Kiswahili
  • Sikiliza taarifa ya Habari
  • RFI kwa Kifaransa

Joseph Kabila DRC

Imechapishwa • Imehaririwa

Wakimbizi 10 wauawa kwa kuchomwa moto mashariki mwa DRC

media
Wanajeshi wa Uganda wakiwa mpakani mwa DRC katika mapmbano dhidi ya Kundi la ADF Photo: AFP Photo/Peter Busomoke

Wakimbizi 10 wameuawa kwa kuchomwa moto Mashariki mwa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo kufuatia mapigano ya kikabila katika jimbo la Kivu Kusini.


Ripoti zinasema kuwa, vijiji kadhaa katika eneo la Balala Kaskazini vilishambuliwa wakati, kabila la Ngumono na waasi wa Forebu kutoka Burundi walipokuwa wanakabiliana.

Kiongozi wa kijiji hicho John Mwimiwa, amethibitisha kutokea kwa mauaji hayo, na kusema wote waliopoteza maisha, waliteketezwa kwa moto.

Hii sio mara ya kwanza kwa mauaji kama haya kuripotiwa Mashariki mwa DRC, kutokana na kuwania ardhi ya makaazi lakini pia sehemu ya kuchunga mifugo.

Makabila ya DRC yamekuwa yakiyashtumu makundi ya waasi kutoka nje ya nchi hiyo, kwa kuwa na njama ya kuwaponya radhi yao kwa lazima. Ukosefu wa usalama umeendelea kusababisha mauaji na maelfu ya watu kuyakimbia makwao Mashariki mwa DRC.