rfi

Hewani
  • RFI Kiswahili
  • Sikiliza taarifa ya Habari
  • RFI kwa Kifaransa
  • Mafuriko yameua watu kumi na nane Iran (idara ya hali ya Dharura)

Madagascar

Imechapishwa • Imehaririwa

Madagascar yakabiliwa na maandamano makubwa

media
Wafanyakazi 400 wa serikali waliandamana Alhamisi, Julai 5, 2018 wakidai kuongezwa mishahara. Sarah T├ętaud/RFI

Wafanyakazi 400 wa serikali wameandamana katika mji mkuu wa Madagascar, Antananarivo wakiitikia wito wa chama cha wafanyakazi. Wafanyakazi hao kutoka wizara ya Posta, Kilimo, Utumishi wa Umma, Elimu ya Taifa wameandamana wakiomba kutafutiwa ufumbuzi kwa madai yao.


Wafanyakazi hao wanadai nyongeza ya mishahara na kuboreshwa kwa mazingira ya kazi.

Wafanyakazi hao wanasema ni miaka 58 hawatendiwi haki, wakati ambapo hali ya maisha inaendelea kuwa mbaya zaidi.

Wafanyakazi wa vyama vya wafanyakazi wengi walidhani kungelifanyika mabadiliko , baada ya Aprili 21. Lakini wameendelea kukata tamaa, amesema Randria Falitsialonina, kiongozi wa chama cha wakaguzi wa ajira.

Majadiliano yanaendelea kuteua wawakilishi watano wa muungano ambao watawasiliana moja kwa moja na Waziri Mkuu na hivyo kutokea kwa mgogoro wa kisiasa. Wakati huo huo, maandamano yanatarajiwa kuendelea Ijumaa wiki hii.