rfi

Hewani
  • RFI Kiswahili
  • Sikiliza taarifa ya Habari
  • RFI kwa Kifaransa

Nigeria Muhammadu Buhari

Imechapishwa • Imehaririwa

Chama tawala chakumbwa na malumbano ya ndani Nigeria

media
Rais wa Nigeria Muhammadu Buhari. REUTERS/Stringer

Nchini Nigeria, baadhi ya wabunge kutoka chama tawala cha All Progressive Congress (APC) wameamua kujitenga na wenzao na kutaka kuunda chama kipya cha siasa.


Hali hiyo inaonyesha mgawanyiko mkubwa unaojitokeza dhidi ya rais Muhammadu Buhari, ambaye anaendelea kukosolewa ndani ya chama chake, ikiwa imesalia miezi isiopungua kumi kabla ya uchaguzi wa urais nchini humo.

Mshirika wa zamani wa Buhari, Buba Galadima alitangaza Jumatano wiki hii kuwa ameunda chama kipya cha Reformed All Progressive Congress (rAPC), na kutoa mwito kwa wabunge na wafuasi wengine wa chama hicho waliojitenga kujiunga naye.

Bw Galadima amemshtumu Muhammadu Buhari kushindwa kutekeleza ahadi zake katika masuala ya usalama na kupambana na rushwa.