rfi

Hewani
  • RFI Kiswahili
  • Sikiliza taarifa ya Habari
  • RFI kwa Kifaransa

DRC UN

Imechapishwa • Imehaririwa

Umoja wa Mataifa wachunguza uhalifu uliotekelezwa Kasai

media
Mtoto anasubiri kupata chakula katika kambi ya wakimbizi wa ndani huko Kaswit, jimbo la Kasai, Juni 7, 2017. JOHN WESSELS / AFP

Baraza la Umoja wa Mataifa la Haki za Binadamu lilikutana Jumanne (Julai 3) huko Geneva na miongoni mwa mafaili yaliyojadiliwa ni pamoja na hali ya usalama inayoendelea Kasaï, nchini Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo.


Mkutano huu umefanyika wiki moja baada ya wataalam wa Umoja wa Mataifa kuwasilisha taarifa kuhusu uhalifu uliofanywa wakati wa machafuko na ukandamizaji kati ya mwaka 2016 na 2017, ambapo baadhi ya vitendo hivyo vinaweza kuelezewa kama uhalifu wa kivita na uhalifu dhidi ya binadamu.

Wataalam wa Umoja wa Mataifa wanakubali kwa urahisi, ripoti yao kuwa "si kamili". Miezi mitano ya uchunguzi, ziara katika maeneo ya matukio na mashahidi 500 na waathirika waliohojiwa hawatoshi kutoa ripoti kamili kuhusu machafuko yaliyotoke huko Grand Kasai kwa zaidi ya mwaka mmoja. Lengo lilikuwa tu "kuweka sawa kwa njia ya haki na isiyopendelea matukio yaliyotokea," amesema Luc Côté, mmoja wa waandishi wa ripoti hiyo.

Lakini kwa mujibu wa wataalamu, uhalifu ulioorodheshwa unaonyesha kiwango cha juu cha vurugu huko Kasai na kuwepo kwa uhalifu wa kivita na uhalifu dhidi ya binadamu uliofanywa kwa sehemu kubwa na vikosi vya jeshi vya Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo, lakini pia na wanamgambo, hasa wafuasi wa Kamuina Nsapu.

Wataalam wanasema wanataka vielelezo vya msingi ili mamlaka nchini DRC ianzishe utaratibu wa kufungua mashtaka. Mashtaka ambayo yamechelewa kuanzishwa, wamesikitika wajumbe wengi wa Baraza la Umoja wa Mataifa la Haki za Binadamu.

Wataalamu sasa wanataka kujua "nini kitakachofanyika na mamlaka ya DR Congo ili kuboresha ufanisi, uwezo wa mfumo wa vyombo vya sheria ,kwa kupata matokeo". Luc Côté, raia wa Canada, ambaye ni mmoja wa wataalam watatu, amesema anatarajia kuwa Baraza la Haki za Binadamu la Umoja wa Mataifa litazingatia kufuatilia uwajibikaji wa mahakama nchini Congo, kwa "kuangalia kinachotokea katika ngazi ya mahakama ".