Pata taarifa kuu
AU-G5 SAHEL-USALAMA

Viongozi wa Umoja wa Afrika waunga mkono kikosi cha G5 Sahel

Sehemu kubwa ya mkutano wa 31 wa umoja wa Afrika nchini Mauritania uligubikwa na mashambulizi ya kigaidi ya hivi karibuni, hususan mashambulizi ya Ijumaa iliyopita katika ngome kuu ya kikosi cha nchi tano zinazo pambana na ugaidi katika ukanda wa Sahel G5 Sahel.

Kikao cha 31 cha Umoja wa Afrika ulifanyika katika jumba hili Nouakchott, Mauritania, 1 Julai 2018.
Kikao cha 31 cha Umoja wa Afrika ulifanyika katika jumba hili Nouakchott, Mauritania, 1 Julai 2018. RFI/Paulina Zidi
Matangazo ya kibiashara

Jumatatu wiki hii rais wa Niger Mahamadou Issoufou ambae ni mwenyekiti wa jumuiya ya G5 Sahel alitembelea chuo cha kijeshi ya G5 Sahel kilichopo nchini Mauritania ambapo alikuwa na ma rais wa Ufaransa, Mali, Tchad, Mauritanie.

Kamanda wa shule hiyo, jenerali Ibrahim Val, amesema nchi 5 za ukanda wa Sahel zilikubaliana kuunda nguvu pamoja kukabiliana na adui ambaye ni ugaidi.

Rais wa Ufaransa Emmanuel Macron ambae yupo katika eneo hilo la ukanda wa Sahel anaendelea na ziara yake barani Afrika, Jumanne hii anazuru nchini Nigeria.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.