rfi

Hewani
  • RFI Kiswahili
  • Sikiliza taarifa ya Habari
  • RFI kwa Kifaransa

Nigeria Muhammadu Buhari

Imechapishwa • Imehaririwa

Polisi waandamana wakidai malipo ya mishahara yao Nigeria

media
Askari wazuia barabara huko Maiduguri, Nigeria, Januari 24, 2015. © AFP

Takribani polisi 2,000 kaskazini mashariki mwa Nigeria, eneo linalokabiliwa na machafuko ya kundi la Boko Haram, wameandamana Jumatatu wiki hii wakidai malipo ya mishahara yao. Duru za kuaminika zinaeleza kuwa polisi hao walifyatua risasi hewani na mabomu ya kutoa machozi.


Polisi hao waandamanaji kutoka kikosi MOPOL, ambao wanahusika na ukaguzi kwenye vituo vya ukaguzi wa polisi na ambao hupiga diria na jeshi, wanadai kulipwa michahara yao ya hadi miezi na kuwa na hali nzuri ya makazi.

Walizuia barabara kuu karibu na makao makuu ya polisi huko Maiduguri, mji mkuu wa Jimbo la Borno, kaskazini mwa Nigeria, wakiimbanyimo mbalimbali kama vile "Tulipe marupurupu yetu au hakutakuwa na amani. "

Maafisa wengine wa polisi walitumwa ili kuzuia waandishi wa habari kutopeperusha au kuripoti kuhusu maandamano hayo, lakini waandamanaji waliingilia kati kujaribu kuwarudisha nyuma, hali ambayo imesababisha makabiliano.

Mmoja wa waandamanaji amliambia shitika la habari la AFP kuwa mara ya mwisho kulipwa, alipokea tu naira 23,000 (sawa na dola 64 au euro 55), sawa na naira 5,000 tu zaidi ya mshahara wa kiwango cha chini wa kitaifa.

"Sehemu kubwa" ya mshahara ilitolewa bila maelezo yoyote, ameongeza. Polisi hawakuweza kutoa fedha kwa familia zao kwa ajili ya chakula au shule.

"Tunawezaje kudumisha usalama wakati tuna njaa na hasira, wakati ambapo hatujaona familia zetu kwa miezi kadhaa na hatuwezi kutimiza majukumu yetu ya msingi kama waume au baba?" amesem ammoja wa waandamanaji. "Uvumilivu wetu umefikia mwisho", ameongeza.