rfi

Hewani
  • RFI Kiswahili
  • Sikiliza taarifa ya Habari
  • RFI kwa Kifaransa

DRC Joseph Kabila CENCO

Imechapishwa • Imehaririwa

DRC yaadhimisha miaka 58 ya uhuru wakati huu CENCO ikitilia shaka uchaguzi wa desemba

media
Rais wa DRC Joseph Kabila REUTERS/Kenny Katombe

Nchi ya Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo, DRC, inaadhimisha kumbukumbu ya miaka 58 ya uhuru wake ilioupata kutoka kwa waliokuwa wakoloni wa taifa hilo nchi ya Ubelgiji, June 30, 1960.


Maadhimisho haya yanafanyika wakati huu Baraza la maaskofu wa kanisa katoliki CENCO likielezea wasiwasi wake kuhusu mchakato wa Uchaguzi unaopangwa kufanyika mwezi desemba mwaka huu.

Akihutubia taifa kupitia televisheni inayomilikiwa na serikali , rais Joseph Kabila amewahakikishia wananchi kuwa uchaguzi huo utafanyika kama ilivyopangwa na CENI huku akiwataka kujitokeza kuunga mkono na kushiriki zoezi la uchaguzi.

Aidha Gavana wa jimbo la kivu kaskazini Julien Paluku amethibitisha kuachwa huru kwa wafungwa 60 kutoka gereza kuu la Goma munzenze,kufuatia msamaha wa raisi katika maadhimisho haya.

Drc inafanya maadhimisho hayo huku ikikabiliwa na changamoto kadhaa ikiwemo umasikini,ukosefu wa usalama katika eneo la mashariki mwa nchi na hofu ya ikiwa uchaguzi mkuu utafanyika kama ilivyopangwa kufanyika Desemba mwaka huu.