rfi

Hewani
  • RFI Kiswahili
  • Sikiliza taarifa ya Habari
  • RFI kwa Kifaransa

CAR DRC ANTIBALAKA

Imechapishwa • Imehaririwa

Wanamgambo 34 wa Anti-Balaka wasafirishwa kutoka DRC

media
Waislam wakikimbilia katika kambi iliyo karibu na Msikiti wa Bangassou huko Jamhuri ya Afrika ya Kati, kufuatia mashambulizi ya kundi la wanamgambo la Anti-Balaka, Agosti 14, 2017. Alexis HUGUET / AFP

Wanamgambo 34 wa Anti-Balaka wa huko Bangassou, kusini-mashariki mwa Jamhuri ya Afrika ya Kati, ikiwa ni pamoja na kiongozi wao "Pino Pino", wamesafirishwa nchini humo kutoka DRC.


Wanamgambo hao walikamatwa nchini DRC mnamo mwezi Mei, Waziri wa Sheria Jamhuri ya Afrika ya Kati amesema.

"Walifika siku mbili zilizopita (Jumatano) na wanazuiliwa Bangui, kwa kusubiri kuhukumiwa" na Mahakama ya Jinai, waziri, Flavin Mbata ameliambia shirika la habari la AFP.

Kesi yao itaanza kusikilizwa mnamo mwezi Julai.

Wanamgambo hawa wa Anti-Balaka wanakabiliwa na mashitaka ya "uhalifu wa kivita, kushirikiana na wahalifu, uhalifu dhidi ya binadamu, kumiliki silaha na vifaa vya kivita kinyume cha sheria, uasi, mauaji na vtisho, uharibifu wa mali za watu wengine na uporaji."

"Pino Pino", mmoja wa viongozi wa kundi la wanamgambo wa Anti-Balaka huko Bangassou, alikamatwa mnamo Mei 16 na wapiganaji wake 33 nchini DRC.

Baadhi yao waliohusika katika shambulio na utekaji nyara wa Walinda amani kutoka Cambodia mnamo mwezi Mei 2017 huko Bangassou, kwa mujibu wa Waziri wa Sheria.

Mwishoni mwa mwezi Januari, "Bere Bere", kiongozi mwingine wa kundi la wanamgambo katika mji huo, alijisalimisha kwa Ujumbe Umoja wa Mataifa nchini Jamhuri ya Afrika ya Kati (Minusca).