rfi

Hewani
  • RFI Kiswahili
  • Sikiliza taarifa ya Habari
  • RFI kwa Kifaransa

Gabon UN

Imechapishwa • Imehaririwa

UN yaitaka Gabon kumuachilia huru waziri wa zamani wa mafuta

media
Rais wa Gabon Ali Bongo. REUTERS/Tiksa Negeri

Kundi wafanyakazi wa Umoja wa Mataifa limeitaka serikali ya Gabon kumuachilia huru waziri wa zamani wa mafuta Etienne Ngoubou, anayeshtumiwa matumizi mabaya ya fedha za umma na ambaye anazuliwa kwa muda wa miezi 17 bila kuhojiwa.


"Bw Ngoubou kunyimwa uhuru ni kinyume cha sheria," kundi la wafanyakazi wa Baraza la Haki za Binadamu la Umoja wa Mataifa linalojihusisha na suala la kufungwa kiholela (GTDA) limebaini katika nakala iliyotumwa katika ofisi ya shirika la habari la AFP leo Jumatano.

Kundi hili limeitaka mamlaka ya Gabon "kumuachilia huru mara moja" Waziri wa zamani wa mafuta, "fidia" na "matibabu sahihi vinahitajika" kwa Bw Ngoubou ambaye ana ugonjwa wa kisukari.

Waziri huyo wa zamani wa mafuta anazuiliwa tangu Januari 12, 2017 kwa kosa la "matumizi mabaya ya fedha za umma" kama sehemu ya Operation iliyoitwa Mamba ikimaanisha "mikono safi" ambayo ilipelekea maafisa wakuu kadhaa kufungwa jela nchini Gabon kwa sababu ya kushtumiwa rushwa.

Ngoubou anashtumiwa kuwa alipitisha mlango wa nyuma Faranga za CFA bilioni 27 (sawa na zaidi ya Euro milioni 44) katika miradi wa umeme na barabara, fedha ambazo zilitolewa na serikali ya Gabon.

Kulinagana na sheria nchini Gabon mthumiwa anawekwa kizuizini kwa muda wa mwaka mmoja kabla ya kesi yake kusikilizwa, wakati waziri wa zamani wa mafuta anafungwa kwa muda wa miezi 17 sasa, kundi hilo la wafanyakazi la baraza la HAki za Binadamu la Umoja wa Mataifa limekumbusha. Kundi hilo linasema kuwa Bw Ngoubou wala wanasheria wake hawana na taarifa za kutosha kuhusu sababu za kifungo chake.