rfi

Hewani
  • RFI Kiswahili
  • Sikiliza taarifa ya Habari
  • RFI kwa Kifaransa

Nigeria Muhammadu Buhari

Imechapishwa • Imehaririwa

Themanini na sita wauawa katika vurugu katikati mwa Nigeria

media
Rais wa Nigeria Muhammadu Buhari amesem aatahakikisha wahalifu wa mauaji ya watu zaidi ya 86 wanafikishwa mahakamani. REUTERS/Dan Kitwood

Watu wasiopungua 86 wameuawa katika mashambulizi yanayodaiwa kutekelezwa na wafugaji wahamaji dhidi ya wakulima katikati mwa Nigeria, eneo linalokabiliwa na machafuko ya kikabila, polisi imesema.


Rais wa Nigeria Muhammadu Buhari ametolea wito kwa wakazi wa eneo hilo kuwa watulivu na gavana wa Jimbo la Plateau, ambapo tukio hilo lilitokea, ametangaza kwamba operesheni kabambe imezinduliwa ili kuwakama wahalifu.

Kwa mujibu wa Mkuu wa polisi Undie Adie, uchunguzi uliofanywa siku ya Jumamosi katika vijiji vya mkoa wa Barikin, katika Jimbo la Plateau, ulipelekea kutambua kwamba jumla ya "watu 86 waliuawa".

Ameongeza kuwa watu sita walijeruhiwa katika mashambulizi haya na nyumba 50 zilichomwa moto.

Kufuatia mashambulizi haya, amri ya kutotoka nje usiku imetangazwa katika maeneo mengi ya jimbo hilo linalokabiliwa kwa siku kadhaa na makabiliano kati ya wakfugaji na wakulima.

Amri ya kutotoka nje usiku imeanza kutumika mara moja "ili kuzuia kuvunjwa kwa sheria na utaratibu," amesema msemaji wa serikali ya jimbo la Plateau, Rufus Bature.

"Mipango ya operesheni imeanza kutekelezwa ili kulinda usalama wa jamii zilizokumbwa na tukio hilo na kuwkamata watu waliohusika na uhalifu huo," amesema Mkuu wa Jimbo la Plateau, Simon Lalong.

"Tutafanya kilio chini ya uwezo wetu ili kulinda jimbo letu mara moja," ameahidi.

Rais Buhari ametolea wito kwa wakaazi wa Jimbo la Plateau kuwa watulivu na kuhakikisha kuwa uwezo wa kila aina utatumiwa ili kuhakikisha wahalifu wanafikishwa mbele ya vyombo vya sheria na kuzuia mashambulizi zaidi.