rfi

Hewani
  • RFI Kiswahili
  • Sikiliza taarifa ya Habari
  • RFI kwa Kifaransa

DRC Marekani Joseph Kabila

Imechapishwa • Imehaririwa

Viongozi waandamizi wa DRC marufuku kuingia Marekani

media
Rais wa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo Joseph Kabila Kabange. REUTERS/Kenny Katombe

Serikali ya Marekani imewachukulia hatua kali maafisa kadhaa wa ngazi ya juu nchini Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo. Maafisa hao wamepigwa marufuku kuingia nchini Marekani kwa sababu ya "kuhusika" kwao katika kesi ya "rushwa kwa lengo la kuzuia mchakato wa uchaguzi," wizara ya mambo ya nje ya Marekani imesema.


Taarifa hiyo ya diplomasia ya Marekani haifafanui idadi au majina au nyadhifa za ya "maafisa" hao kuhusika.

Ikihojiwa na shirika la habari la AFP, Wizara ya mambo ya nje ya Marekani imekataa kutaja majina ya maafisa hao, ikieleza kuwa ni "orodha binafsi" iliyofanywa "kwa misingi ya masuala ya sera za kigeni" chini ya sheria ya Marekani.

"Hata kama watu hao hawakutajwa majina hadharani, tunaamini kwamba hii inapeleka ujumbe muhimu: rushwa haikubaliki, huathiri taasisi za nchi na ina madhara makubwa," afisa mmoja kutoka wizara ya mamabo ya nje ya Marekani amesema.

"Serikali ya Marekani imedhamiria kupambana na rushwa, kusaidia uchaguzi wa kuaminika na kupelekea kuna kuepo na zoezi la kwanza la kukabidhiana madaraka kwa amani na katika mfumo wa kidemokrasiakatika historia ya nchini DRC".

Marekani imetoa wito wa kufanyika "uchaguzi wa kuaminika na wa wazi na utakaofanyika kwa muda muafaka mnamo mwezi Desemba 2018.

Rais Joseph Kabila, 47, madarakani tangu mwaka wa 2001, ambaye alichaguliwa mwaka 2006, na mwaka 2011, haiwezi kuwania kwa muhula mwengine kulingana na Katiba ambayo inaweka mihula miwili kwa rais aliyechaguliwa.