rfi

Hewani
  • RFI Kiswahili
  • Sikiliza taarifa ya Habari
  • RFI kwa Kifaransa

DRC Joseph Kabila

Imechapishwa • Imehaririwa

Bunge lajadili sheria ya kuwalinda marais waliostaafu DRC

media
Aubin Minaku, Spika wa bunge, DRC. RFI/Habibou Bangré

Baraza la wawakilishi na bunge la Seneti nchini DRC linakutana leo Jumatano katika kikao maalum, kwa ombi la Rais Joseph Kabila, ili kutathmini sheria itakayowalinda marais wa zamani" wa nchi hiyo, kwa mujibu wa televisheni ya serikali.


"Bunge la taifa linakutana katika kikao maalum" kuanzia Juni 20 hadi Julai 19, Minaku Aubin, Spika wa Bunge ameandika katika taarifa iliyosomwa kwenye radio na televisheni vya serikali (RTNC) usiku wa kuamkia Jumatano wiki hii.

Pointi sita zitajadiliwa katika kikao hicho maalum, ikiwa ni pamoja na "sheria inayowahusu marais wa zamani wa waliochaguliwa" ikiwa imesalia miezi sita kabla ya kufanyika uchaguzi wa urais unaotakiwa kumchagua mrithi wa Rais Kabila, ambaye muhula wake unatamatika Desemba 20, 2016.

Tangu mwaka 1960, zoezi la kukabidhiana madaraka kwa amani halijawahi kushuhudiwa nchini DRC.

Bunge la taifa pia litatathmini ripoti ya kila mwaka ya tume inayohusika na kuandaa uchaguzi nchini DRC na faili kuhusu uteuzi wa baadhi ya wajumbe watakaochukua nafasi ya wengine kwenye tume hiyo.

Wabunge na Maseneta pia watajadili sheria kuhusu ulinzi na uwajibikaji wa wanaharakati wa haki za binadamu.

Makao makuu ya serikali , Gombe, Kinshasa JUNIOR KANNAH/AFP