Pata taarifa kuu
Viongozi wa makundi yanayohasimiana Sudani Kusini kukutana Jumatano

Viongozi wa makundi yanayohasimiana Sudani Kusini kukutana Jumatano

Rais wa Sudan Kusini Salva Kiir atakutana na Makamu wa zamani wa rais Riek Machar Jumatano wiki hii kujadili namna ya kuanzisha upya mchakato wa amani unaotarajiwa kumaliza mgogoro unaoikabili nchi hiyo tangu mwaka 2013, waziri wa mambo ya nje wa Ethiopia amesema Jumanne wiki hii.

Kiongozi wa waasi, Riek Machar (kulia) na rais wa Sudani Kusini, Salva Kiir (kushoto) Mei 9 mwaka 2014.
Kiongozi wa waasi, Riek Machar (kulia) na rais wa Sudani Kusini, Salva Kiir (kushoto) Mei 9 mwaka 2014. REUTERS/Goran Tomasevic
Matangazo ya kibiashara

Mkutano wa siku ya Jumatano kuhusu Sudan Kusini utafanyika chini ya usimamizi wa Waziri Mkuu (Ethiopia) Abiy Ahmed ili kuzuia pengo kati ya Rais Salva Kiir na Riek Machar," Wizara ya mambo ya nje ya Ethiopia imesema.

Nakala hiyo inaongeza kuwa Riek Machar anatarajiwa Addis Ababa Jumatano wiki hii.

Awali serikali ya Sudani Kusini ilitaka mkutano wa ana kwa ana kati ya rais Salva Kiir na hasimu wake Riek Machar ufanyike katika taifa lisilo na maslahi na upande wowote kati ya viongozi hao.

Siku ya Jumatatu wiki hii Waziri wa habari na msemaji wa serikali ya Juba Michael Makuei, amesema mkutano wa kihistoria unaweza kufanyika katika taifa lolote kutokana na kuwepo mvutano wa kimaslahi miongoni mwa mataifa ya jumuiya ya iGAD ambayo yamekuwa yakiandaa mazungumzo hayo.

Miongoni mwa mataifa ambayo yamewahi kuandaa mazungumzo hayo ni pamoja na Ethiopia na Kenya lakini hivi karibuni na Sudani ya khartoum nayo ilitangaza kuwa tayari kuandaa.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.