Pata taarifa kuu
MALI-UFARANSA-GASAMA-USALAMA

Mamadou Gassama: Nimefurahishwa sana kurudi nyumbani Mali

Mamadou Gassama, raia wa Mali aliyemwokoa mtoto mchanga katika jumba la orofa nchini Ufaransa mwezi Mei, yuko nyumbani Mali na alipokelewa kama shujaa.

Rais wa Mali Ibrahim Boubacar Keïta (kulia) na Mamoudou Gassama Juni 18 huko Bamako.
Rais wa Mali Ibrahim Boubacar Keïta (kulia) na Mamoudou Gassama Juni 18 huko Bamako. Michele CATTANI / AFP
Matangazo ya kibiashara

Gassama ambaye alikuwa mhamiaji haramu nchini Uaransa, amepewa jina la Spiderman tayari amepewa uraia na nchi ya Ufaransa na mwisho wa mwezi huu anatarajiwa kutia saini mkataba na jeshi la kuzima moto nchini humo.

Aidha, Gassam ambaye ameelezwa kama shujaa, alikutana na rais wa Mali Ibrahim Boubacar Keïta.

Mamoudou Gassama amesema amefurahishwa sana kurudi kwao Mali kutembea.

Rais wa Ufaransa Emmanuel Macron binafsi alimshukuru Bw Gassam na kumuahidi kuwa atapa uraia wa Ufaransa.

Video ya Mamoudou Gassam akimuokoa mtoto ilisambaa sana kwenye mitandao ya kijamii.

Bw Gassama, 22, alivuka bahari ya Mediterranean kwa mashua ya wahamiaji mwezi Septemba mwaka 2014.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.