rfi

Hewani
  • RFI Kiswahili
  • Sikiliza taarifa ya Habari
  • RFI kwa Kifaransa

Mali Ibrahim Boubacar Keita Mauaji

Imechapishwa • Imehaririwa

Makaburi ya halaiki yagunduliwa Nantaka na Kobaka

media
Miili hiyo ilipatikana katika makaburi mawili, kilomita chache kutoka miji miwili ya Nantaka na Kobaka. Miili kumi na mitatu katika shimo moja, saba katika chimo nyingine na miili mitano katika shimbo la tatu. © RFI

Watu wengi wanajiuliza kilichotokea Juni 13 huko Nantaka na Kobaka, maeneo mawili nchini Mali, sio mbali na Mopti, upande wa pili wa Mto Nige. Makaburi matatu ya halaiki yaligunduliwa kilomita chache kutoka miji hiyo miwili.


Miili ishirini na mitano kwa jumla; Miili ishirini na tano ya watu kutoka jamii ya Fulani. Jeshi linahusishwa na mauaji hayo, kwa mujibu wa mashahidi.

Shahidi mmoja, mchungaji aliyehojiwa na RFI, anasema kile alichoona Nantaka, kabla ya kugunduliwa kwa miili hiyo, siku ya pili, "... katika shimo". "Niliona wanajeshi, nliona wajeshi ...", anasema, akizungumzia malori. Kwa mujibu wa mchungaji huyu, jeshi lilikamata wanaume. "lilikua likienda nyumba kwa nyumba," anasema. Aliweza kujificha nje ya mji. Ilikuwa tarehe 13 Juni.

Chanzo kingine, mjini Mopti kinasema kuwa vikosi vya jeshi, FAMA, waliondoka kwa lori kutoka Nantaka na Kobaka na watu wote waliokamatwa. Jeshi hilo linadaiwa kuwa liliwaachia watu kutoka jamii ya Songhai, watu weusi kutoka jamii ya Tamasheq na Bozo, wakendelea kuwashikilia watu 25 kutoka jamii ya Fulani (Wafugaji).

Miili hiyo ilipatikana katika makaburi mawili, kilomita chache kutoka miji miwili ya Nantaka na Kobaka. Miili kumi na mitatu katika shimo moja, saba katika chimo nyingine na miili mitano katika shimbo la tatu. Orodha ya majina ilifichuliwa. Kati ya watu 25, 21 ni kutoka mji wa Nantaka. Wengine waliishi katika vijiji vilicyo karibu na mji huo.

Wakihojiwa na RFI.msemaji wa serikali na waziri wa ulinzi wamesema uchunguzi umeanzishwa. Mkuu wa majeshi anahojiwa. Lakini viongozi hawa wawili wanasema kuwa "jeshi halijahusika katika matukio haya, ikiwa ni kweli yalitokea".