rfi

Hewani
  • RFI Kiswahili
  • Sikiliza taarifa ya Habari
  • RFI kwa Kifaransa

Afrika Kusini Mauaji Uislam

Imechapishwa • Imehaririwa

Watu 2 wauawa kwa kuchomwa kisu msikitini Afrika Kusini

media
Sala katika Msikiti wa Nizamiye huko Midrand, Johannesburg, Mei 16, 2018 AFP

Watu wawili wameuawa kwa kuchomwa kisu wakati wa sala ya Alfajiri Alhamisi wiki hii katika msikiti wa Malmesbury kusini-magharibi mwa Afrika Kusini. Mshambuliaji ameuawa na polisi.


Tukio hili linatokea ndani ya mwezi mmoja baada ya shambulio jingine kama hili kutokea katika eneo la ibada kwa waumini wa Kiislamu nchini Afrika Kusini.

Baada ya kupewa taarifa na waumini, polisi wliwasili mapema asubuhi katika msikiti huo wa jiji, kilomita sitini kaskazini mwa mji wa kitalii wa Cape, na kugundua miili ya watu wawili waliofariki kwa majeraha baada ya kuchomwa kisu.

Msemaji wa polisi katika mkoa huo, Noliyoso Rwexana ameliambia shirika la habari la AFP kwamba "Mtuhumiwa mwenye umri wa miaka thelathini, ambaye alijihami kwa kisu, aliwashtumu polisi kuhusika na vifo hivyo walipokuwa wakijaribu kumtaka ajisalimishe." "Alipuuzia amri hiyo, na kujaribu kushambulia polisi. Wakati huo polisi hawakusita kujihami na kumpiga risasi na kufa papo hapo."

Mshambuliaji alijeruhi watu wengine wawili, ambao wamelazwa hospitalini, msemaji wa polisi amesema.

Kwa mujibu wa vyombo vya habari vya Afrika Kusini, mshambuliaji, alikua raia wa Somalia, lakini polisi imejizuia kutoa maelezo yoyote kuhusiana na taarifa.

Sababu ya shambulizi la awali hazijatolewa, lakini kwa mujibu wa polisi, shambulizi hilo lilikua na "dalili za ugaidi".

Kiongozi wa jumuiya ya Waislam nchini Afrika Kusini, Moulana Aftab Haider, amesema kwamba shambulizi hilo lilickua lilikua na dadili zinazofanana na zile "za kundi la makundi ya kigaidi kama (kundi) la Islamic State".