rfi

Hewani
  • RFI Kiswahili
  • Sikiliza taarifa ya Habari
  • RFI kwa Kifaransa

DRC CAR ICC Jean-Pierre Bemba

Imechapishwa • Imehaririwa

ICC kuwasaidia waathirika wa vitendo vya wapiganaji wa Bemba

media
Makao makuu ya Mahakam ya Kimataifa ya Uhalifu ICC. Wikip├ędia

Mahakama ya kimataifa ya uhalifu wa kivita ICC imeanzisha mfuko wa fedha wenye thamani ya dola milioni 1.8 kwaajili ya kuwasaidia waathirika wa vitendo vya wapiganaji wa aliyekuwa makamu wa rais wa DRC Jean-Pierre Bemba.


Mfuko huu umetangazwa baada ya Bemba kufutiwa mashtaka ya makosa ya kivita na dhulma dhidi ya binadamu na fedha hizo zitatolewa kwa waathirika walioteswa na wapiganaji wa Bemba nchini jamhuri ya Afrika ya Kati.

ICC inasema makosa yaliyotendeka nchini Jamhuri ya Afrika ya Kati hayajasahaulika.

Kuachiwa huru kwa Bemba hata hivyo kumeacha hasira toka kwa baadhi ya raia ambao wanaona licha ya kuwa hakuwepo nchini Jamhuri ya Afrika ya Kati lakini anawajibika kwa kuwatuma askari wake kutekeleza vitendo vya kikatili.

Baadhi ya raia na wanasiasa nchini DRC wameonesha kufurahishwa na uamuzi wa majaji wa mahakama ya kimataifa ya uhalifu wa kivita ICC, kumwachia huru kwa masharti aliyekuwa makamu wa rais Jean-Pierre Bemba Gombo baada ya kufutiwa makosa ya uhalifu wa kivita na dhulma dhidi ya binadamu.