rfi

Hewani
  • RFI Kiswahili
  • Sikiliza taarifa ya Habari
  • RFI kwa Kifaransa

Tanzania ICGLR

Imechapishwa • Imehaririwa

Wadau kutoka idara za Mahakama kutoka ICGLR wakutana Dar es Salaam

media
Mkutano wa ICGLR, uliofanyika Kampala, Uganda Agosti 7, 2012. REUTERS/Edward Echwalu

Wadau kutika idara za Mahakama kutoka mataifa ya ukanda wa Maziwa Makuu wanakutana leo na kesho jijini Dar es salaam nchini Tanzania. Mkutano huu wa ngazi ya juu wa Jumuiya ya nchi za Maziwa Makuu unaohusu ushirikiano katika masuala ya makosa ya jinai, umeanza Jumatano wiki hii.


Mkutano huo unatarajiwa kutoka maazimio ya namna ya kutekeleza mikataba na makubaliano yaliyopo ya ushirikiano katika ukanda wa Maziwa Makuu.

Kikao hiki cha Dar es salaam kinatarajiwa kutoa nafasi kwa nchi wanachama kutimiza ahadi zao za kisheria katika utekelezwaji wa ushirikiano huo.

Ushirikiano huu, unatarajiwa kuziepusha nchi za ICGLR kuwalinda au kuwatetea watu wanaojihisha na makosa dhidi ya uhalifu wa kibiandamu, mauaji ya kimbari miongoni mwa makosa mengine ya jinai.

Balozi Maalumu wa Umoja wa Mataifa anayehusika na masuala ya nchi za Maziwa Makuu Said Djinnit, akizungumza katika ufunguzi wa mkutano huo, amesema kuwa viongozi wa eneo la Maziwa Makuu wameazimia kupambana na suala la wahalifu kuepuka adhabu, hivyo kuimarisha ushirikiano wa kimahakama kama njia moja wapo ya kupunguza uhalifu katika eneo hilo.

Mkurugenzi msaidizi wa mashtaka, Fredrick Manyanda, amesema kikubwa kitakachojadiliwa ni namna ya kuimarisha ushirikiano.