Pata taarifa kuu
EQUATORIAL GUINEA-SIASA

Rais wa Equatorial Guinea ataka kufanyika kwa mjadala wa kitaifa

Rais wa Equatorial Guinea Teodoro Obiang Nguema amwataka kufanyika wanasiasa na wadau mbalimbali kushiriki mjadala wa kitaifa nchini humo, hatua inayokuja baada ya kushindikana kwa jaribio la mapinduzi na operesheni ya kuwakamata wapinzani.

Rais wa Equatorial Guinea Teodoro Obiang Nguema Mbasogo, anataka kuona kunafanyika mjadala wa kitaifa utakaojumuisha pia wanasiasa, mjadala ambao sasa umepangwa kufanyika mwezi Julai..
Rais wa Equatorial Guinea Teodoro Obiang Nguema Mbasogo, anataka kuona kunafanyika mjadala wa kitaifa utakaojumuisha pia wanasiasa, mjadala ambao sasa umepangwa kufanyika mwezi Julai.. REUTERS/Amr Abdallah Dalsh
Matangazo ya kibiashara

Katika hotuba aliyoitoa usiku wa kuamkia Jumatano hii, rais Nguema amesema anataka kuona kunafanyika mjadala wa kitaifa utakaojumuisha pia wanasiasa, mjadala ambao sasa umepangwa kufanyika mwezi Julai.

Rais Nguema amewataka raia wake wanaoishi uhamishoni kurejea nyumbani akisema amani na utulivu inategemea pia ushiriki wao.

Mwanzoni mwa mwezi Januari mwaka huu rais wa Equatorial Guinea alisema kuwa jaribio la mapinduzi dhidi ya serikali yake lilipangwa nchini Ufaransa nchi hiyo ikipaza sauti yake kuwa raia wake wanaoishi barani Ulaya walihusika.

Akizungumza na waandishi wa habari, Waziri wa Mambo ya Kigeni wa Equatorial Guinea Agapito Mba Makuy alisema jaribio hili halina uhusiano wowote na serikali ya Ufaransa na kwamba watashirikiana na nchi hiyo pindi watakapopata taarifa kamili.

Mokuy alisema kuwa kutokana na jaribio hili nchi yake imesitisha utolewaji wa bure wa visa za kuingia nchini humo kwa raia kutoka mataifa sita ya Afrika ya kati na Magharibi.

Wakati huo serikali ilisema kuwa mamluki 27 walikamatwa na vyombo vya dola na wengine zaidi ya 150 wanasakwa kwenye eneo la mpaka wa nchi hiyo na Cameroon.

Nchi ya Equatorial Guinea imekuwa ikiongozwa na familia ya Teodoro Obiang Nguema toka mwaka 1979.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.