rfi

Hewani
  • RFI Kiswahili
  • Sikiliza taarifa ya Habari
  • RFI kwa Kifaransa

DRC Joseph Kabila Bruno Tshibala

Imechapishwa • Imehaririwa

Bruno Tshibala: Kabila hatogombea urais mwaka huu

media
Rais wa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo Joseph Kabila katika mkutano na waandishi wa habari katika ikulu mjini Kinshasa, Januari 26, 2018. REUTERS/Kenny Katombe

Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo Bruno Tshibala amesema rais Jospeh Kabila hatawania urais, wakati wa Uchaguzi Mkuu mwezi Desemba.


Tshibala, amesema kuwa Kabila ambaye muhula wake ulikamilika mwaka 2016, ataheshimu Katiba.

Hata hivyo, wanasiasa wa upinzani wamekuwa wakisema, wanamtaka rais Kabila mwenyewe kutanagza kuwa hatawania tena na kwenda kinyume na katiba ya nchi hiyo.

Hivi karibuni mabango yenye picha ya rais Joseph Kabila, yakiwa na maandishi kuwa Kabila ni "mgombea" wa kiti cha urais katika uchaguzi wa Desemba 23 yalizua hali ya hasira miongoni mwa wanasiasa wa upinzani na mashirika ya kiraia nchini humo.

Mabango hayo yaliyobuniwa na wafuasi wa chama tawala cha PPRD yameonekana katika maeneo ya umma, kama vile Soko la Lalu, katika wilaya ya Binza Delvaux, magharibi mwa jiji kuu Kinshasa.

Wadadisi wa mambo wanaona kuwa mpango huo ulioanzishwa na chama hicho ni “mkakati hatari" kwa mchakato wa uchaguzi nchini humo.

Uchaguzi mkuu nchini DRC umepangwa kufanyika Mnamo mwezi Desemba mwaka huu.

Lakini wanasiasa nchini DRC hawajaafikiana kama kweli uchaguzi huo utafanyika Rais Kabila akiwania kwa muhula mwingine.

Jambo hilo limekua likizua sintofahamu, lakini mpaka sasa Rais Joseph Kabila hajazungumzia nia yake ya kuwania au la katika uchaguzi huo.