rfi

Hewani
  • RFI Kiswahili
  • Sikiliza taarifa ya Habari
  • RFI kwa Kifaransa

DRC ICC Jean-Pierre Bemba

Imechapishwa • Imehaririwa

Hatima ya Bemba kuachiliwa au la kujulikana Jumatano hii

media
Makao makuu ya Mahakam ya Kimataifa ya Uhalifu ICC. Wikipédia

Hatimaye majaji wa Mahakama ya Kimataifa ya Uhalifu (ICC) wameahidi kutoa uamuzi wao kuhusu kuachiliwa huru kwa dhamana kwa aliyekua kiongozi wa kivita nchini DRC, na makamu wa zamani wa rais, Jean-Pierre Bemba ifikapo Jumatao wiki hii.


Hatua hiyo imechukuliwa Jumanne wiki hii katika kikao cha majaji ambacho kilidumu saa moja.

Baada ya kufutiwa makosa katika kesi kubwa katika uhalifu wa kivita na uhalifu ulitekelezwa nchini Jamhuri ya Afrika ya Kati, aliyekuwa makamu wa rais wa Congo ameomba kuachiliwa nchini Ubelgiji kwa kusubiri hukumu nyingne katika kesi ya pili. Anakabiliwa na kifungo cha miaka mitano, adhabu ambayo tayari ametumika. "Tunafahamu kwamba uamuzi wa siku ya Ijumaa uliwashangaza baadhi ya watu, lakini hukumu hii ni ya mwisho na vigezo vya kuendelea kumshikilia kizuizini hakuna," amesema mwanasheri wa Jean-Pierre Bemba. Kwa upande wa ofisi ya mwendesha mashitaka, kesi hizi mbili ziko tofauti, na kesi hii ya pili ina 'uzito wake.' Upande mashtaka umewaomba majaji kutoshinikizwa kumuachilia huru.

Hata hivyo wataalamu wa masuala ya sheria za kimataifa wanasema kuna uwezekano mkubwa kiongozi huyo wa zamani wa kivita kuachiliwa huru.

Ofisi ya mwendesha mashitaka ya ICC ilishindwa kutoa ushahidi tosha unaomuhusisha Bemba katika uhalifu uliotekelezwa na wapiganaji wake nchini Jamhuri ya Afrika ya Kati.

Jean-Pierre Bemba mwenye umri wa miaka 55 alikataa rufaa mwezi Juni 2016 kwa uamuzi wa ICC kumpata na kosa la kuhusika katika mlolongo wa mauaji na ubakaji, vitendo vilivyofanywa na wanamgambo wake wa kundi la waasi la MLC, nchini Jamhuri ya Afrika ya Kati kati ya mwezi Oktoba 2002 na mwezi Machi 2003.

Katika muda wa miezi mitano, wapiganaji 1,500 wa MLC waliua, waliiba na kubaka nchini Jamhuri ya Afrika ya Kati, ambapo walikwenda kumsaidia rais Ange-Félix Patassé dhidi ya jaribio la mapinduzi lililoendeshwa na Jenerali François Bozizé.

Kesi yake iliyofunguliwa mjini Hague mnamo mwezi Novemba 2010, ilikuwa ni ya kwanza ya ICC iliyolenga ubakaji na unyanyasaji wa kijinsia kama uhalifu wa kivita na kumuhusisha kiongozi mkuu wa jeshi kutokana na uzembe kwa watu waliokua chini ya uongozi wake

Hukumu ya kifungo cha miaka 18 ni hukumu kubwa kabisa kuwahi kutolewa na mahakama hiyo ilianzishwa mwaka 2002 ili kuhukumu uhalifu mbaya unaotekelezwa duniani.

Jean-Pierre Bemba mahakamani ICC, Hague, Uholanzi, Julai 4, 2008. (Photo : Reuters)