rfi

Hewani
  • RFI Kiswahili
  • Sikiliza taarifa ya Habari
  • RFI kwa Kifaransa

Msumbiji Mauaji

Imechapishwa • Imehaririwa

Watu zaidi ya 5 wauawa katika shambulizi Msumbiji

media
Polisi wa msumbiji wakipiga doria. AFP PHOTO / FERHAT MOMADE

Visa vya mauaji vinaendelea kushuhudiwa nchini Msumbiji, mauaji ambayo wanahusishwa wanamgambo wa Kiislamu. Watu zaidi ya 5 waliuawa Jumatano usiku wiki hii kwa kukatwa na mapanga na visu kaskazini mashariki mwa nchi hii.


"Kulitokea shambulizi jipya" katika jimbo la Cabo Delgado, msemaji wa polisi amnbaye hakutaja jina lake ameliambia shirika la habari la AFP. "Kundi hilo lililoendesha mashambulizi katika vijiji jirani limeshambulia kijiji kingine jana (Jumatano) saa tsatu usiku, shambulizi amblo liligharimu maisha ya watu watano," ameongeza.

Washambuliaji walikuwa walijihami kwa mapanga na visu, amesema, huku akibaini kwamba waliharibu nyumba kadhaa.

Tukio hilo lilitokea katika kijiji cha Namaluco, kilomita zaidi ya mia moja kaskazini mwa Pemba, mji mkuu wa Cabo Delgado.

Shambulizi lililosababisha vifo hili ni la tatu tangu mwishoni mwa mwezi Mei katika jimbo hilo.