rfi

Hewani
  • RFI Kiswahili
  • Sikiliza taarifa ya Habari
  • RFI kwa Kifaransa

DRC

Imechapishwa • Imehaririwa

Visa vya utekaji nyara kwa watoto vyakithiri Kivu Kusini

media
Mji wa Bukavu Mashariki mwa DRC. www.rfi.fr

Kuanzia mwezi Januari 2017 hadi mwezi Mei 2018, karibu watoto 85 walitekwa nyara katika mkoa wa Kivu Kusini, mashariki mwa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo. viongozi tawala katika mkoa huo wamethibitisha hali hiyo.


Mashirika ya haki za binadamu yameiomba serikali kukomesha hali hii, ambayo inachingia kwa mdororo wa usalama nchini.

Kiongozi wa shirika la haki za binadmu la ASADHO, Joshua Blaise Mukubwa, anasema hali hii inatisha, huku akiwalamu viongozi wa mkoa wa Kivu Kusini kushindwa kudhibiti hali hii.

Kwa mujibu wa Bw Mukubwa maeneo ya pwani ya mkoa wa Kivu Kusini, karibu na Ziwa Kivu na Ziwa Tanganyika, ni maeneo yaalioathirika zaidi na visa hivi vya utekaji nyara kwa watoto ambavyo vilianza kuongezeka tangu mwanzoni mwa mwaka 2018.

Wakati huo huo Idara ya uhamiaji nchini DRC imechukua hatua kwa mtu yeyote anayetaka kuvuka mpaka na mtoto mdogo.