rfi

Hewani
  • RFI Kiswahili
  • Sikiliza taarifa ya Habari
  • RFI kwa Kifaransa

DRC ICC Jean-Pierre Bemba

Imechapishwa • Imehaririwa

Hatima ya Jean-Pierre Bemba kujulikana Ijumaa

media
Jean-Pierre Bemba anashtumiwa kushindwa kuzuia uhalifu uliokua ukitekelezwa na wapiganaji wake Jamhuri ya Afrika ya Kati. AFP/MICHAEL KOOREN

Mahakama ya Kimataifa ya Jinai (ICC) inatarajia kutoa uamuzi wake Ijumaa wiki hii kuhusu rufaa dhidi ya Makamu wa zamani wa rais nchini DRC, Jean-Pierre Bemba, ambaye alihukumiwa miaka 18 jela kwa kosa la uhalifu wa vita.


Jean-Pierre Bemba mwenye umri wa miaka 55 alikataa rufaa mwezi Juni 2016 kwa uamuzi wa ICC kumpata na kosa la kuhusika katika mlolongo wa mauaji na ubakaji, vitendo vilivyofanywa na wanamgambo wake wa kundi la waasi la MLC, nchini Jamhuri ya Afrika ya Kati kati ya mwezi Oktoba 2002 na mwezi Machi 2003.

Katika muda wa miezi mitano, wapiganaji 1,500 wa MLC waliua, waliiba na kubaka nchini Jamhuri ya Afrika ya Kati, ambapo walikwenda kumsaidia rais Ange-Félix Patassé dhidi ya jaribio la mapinduzi lililoendeshwa na Jenerali François Bozizé.

Kwa mujibu wa majaji, Jean-Pierre Bemba "aliongoza mashambulizi makubwa dhidi ya raia wasiokua na hatia" wakati ambapo"familia mbalimbali zililengwa na mashambulizi hayo.

Bw Bemba, ambaye alikuwa anatambua hali hiyo, "alishindwa kuchukua hatua zinazohitajika na za ufanisi kuzuia uhalifu huu usitekelezwi na waasi wake au kuwazuia", Mahakama imlisisitiza.

Kesi yake iliyofunguliwa mjini Hague mnamo mwezi Novemba 2010, ilikuwa ni ya kwanza ya ICC iliyolenga ubakaji na unyanyasaji wa kijinsia kama uhalifu wa kivita na kumuhusisha kiongozi mkuu wa jeshi kutokana na uzembe kwa watu waliokua chini ya uongozi wake

Hukumu ya kifungo cha miaka 18 nihukumu kubwa kabisa kuwahi kutolewa na mahakama hiyo ilianzishwa mwaka 2002 ili kuhukumu uhalifu mbaya unaotekelezwa duniani.